July 7, 2007

Je Mhariri wako aweza tumia picha hii? Hii ni kama kuwakumbusha wadau wenzangu ktk fani, juzi wakti twampokea Rais wa Msumbiji pale airport kuna kitu kilijitokeza kuhusiana na utendaji wetu na ushirikiano na hawa "rafiki zetu", sote tuliona kajukwaa kalikoweka kwa ajili yetu na kwa kweli hakakutumika na yeyote kati yetu kwani haikuzingatia mahitaji yetu yoyote ya utendaji wa kazi zetu, sote twafahamu kuwa photo-graphy ni kuchora kwa mwanga, hilo ndilo la msingi na namba moja ktk fani yetu, mengine lakini ambayo pia ni muhimu "angle" sasa kijukwaa kile situ kwamba kilikuwa kinyume na mwamga bali pia nyuma ya umati wa akinamama ambao walijitokeza kumpokea mgeni huyo, yaani kamera zimefichwa nyuma ya migongo ya kinamama hao na hawa rafiki zetu kwao ilikuwa ni sahihi kabisa. Wote ilibidi kujaribu kutafuta angle nzuri zaidi ili kupata picha na kuacha kajukwaa kale ndipo "rafiki zetu" hawa wakaanza kusukumana nasi, Lakini bahati nzuri Rais wetu anajua nini tunafanya na unuhimu wa kile tufanyacho hivyo hakupendezwa na hali ile ilibidi kuinguilia kati kwa kuwafokea "rafiki zetu" kwamba kwanini wanatuzuia na je tutapataje picha ambazo ni kumbukumbu muhimu kwa taifa letu. Ukweli ni jambo la aibu sana kwa hawa "rafiki zetu" kumwacha Mh Rais JK badala ya kupokea mgeni wake muhimu aanze kufokea au kuwakumbusha wasaidizi wake hawa majukumu yao, hii maana yake ni kwamba wameshindwa kumsaidia Rais hata kufikia kufanya kazi yao. ukweli ni kuwa pamoja wahariri wetu wanaweza kuwa hawajui shuruba au mizengwe tuipatayo tukiwa ktk kazi kama hizi, lakini hakuna ambaye atakuwa tayari kutumia picha ya migongo ya watu eti tu kwa sababu uliwekwa au kupangwa kukaa sehemu isiyozingatia umuhimu wa kazi yako, au waweza mpelekea mhariri wako picha kama iyo hapo juu? Yaweza kuwa picha nzuri, kwa maana ya mwanga na labda moment lakini caption yake itakuwaje? Katika hali yoyote iko aja ya "rafiki zetu" hawa kufika mahali wakaelewa umuhimu wa kazi za wengine na hivyo kutupa nafasi ili tutekeleze majukumu yetu pasi na mikwaruzano kama vile ilivyo kwa wenzetu niliyowahi wanyesha hapa. Pia nadhani iko aja ya kuwa na mtu anayejua umuhimu na mazingira bora ya upatikanaji wa picha wakati wa upangaji na uandaaji wa shughuri kama hizi ili kuepuka kumfanya Mh Rais kuwa anaingilia kati kila wakati kwani anashughuri nyingi na za muhimu zaidi ya kuangalia kuwa kwanini twasukumana au hatupati picha. Tatizo moja ambalo nimeliona ni kuwa hawa "rafiki zetu" huwa wanakuja kwa nia moja kutudhibiti, yaani kazi yao ni kudhiti wapiga picha na si kuwafanya wapiga picha wafanye kazi zao kwa utaratibu. "Rafiki zetu" naomba wabadili hiyo mind set yao na watengeneze mazingira mazuri ya sisi kufanya kazi na wao ndivyo watakavyokuwa na kazi ndogo zaidi ya kutudhiti bali itakuwa kutudhitisha.

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...