July 2, 2007

"Halloo!! shikamoo kaka, habari za leo, samahani nakuomba uje leo saa tano na nusu pale Ilala Boma CCM kutakuwa na............." Hii ilikuwa ni sauti nyororo ya kubembeleza ambayo haikuwa ikiitaji utambulisho wowote uisikiapo mara upokeapo simu hasa kwa wanahabari wenzangu, ni sauti ya aina yake ambayo huwezi ifananisha na ingine au kuikosea na kama vile aliyekuwa anaitoa alikuwa akijua hivyo kwani ni aghalabu sana kusikia akijitambulisha. Leo hii eti naambiwa sintoiskia tena abadani sauti hii? siamini!! eti ya kwamba imezimika ghafla kama kibatali au mshumaa uzimwao kwa hata kwa upope hafifu? hapana haiwezekani!! ati sasa waitwa marehemu? no haiwezekani!! mbona hukutupigia? mbona husitujulishe wadau wako kwa ile sauti yako nyororo ya kuwa watutoka? mbona husituage wadau wako Amina? Mbona ni mapema mno? yaani ndo kwanza jua lachomoza nawe waondoka? hukututendea haki washikadau. Wanasema Mungu alikupenda zaidi? nakataa kuamini,, je ni kweli alikupenda mno kuliko vijana ulioapa kuwatetea na wakakuchagua kuwawakilisha? ni kweli alikupenda kuliko mwanao unayemwacha bila mama ktk umri mdogo hivi? Akili yangu ya kawaida yakataa kuamini, niwieni radhi kwa kutokuamini kwangu, pia nafahamu kazi ya Mungu haina makosa, lakini haa! sawa tutafanyaje!! Imenichukua mda mrefu kuandika tanzia hii kwa kutoamini kwangu, nikidhani labda niko ktk ndoto ndefu na kwamba uenda nikiamka nitasikia tena sauti ile tamu ikinialika kwa ili au lile, sauti toka ktk sura ya tabasamu isiyo jua kununa, Lakini wapi siku zimepita na bado nasoma tanzia toka sehemu mbali mbali nami nalazimika kuamini japo kwa shingo upande kwamba ni kweli umetutoka Amina, waudaku walikufanya mradi, mamilion mengi wametengeneza kwa kupitia sura yako, kiasi najiuliza wapi watapata tena A.C mwingine? je ni nini wamekulipa A.C? Yako mengi mno ya kuandika juu yako lakini itoshe kusema tu kwamba ulikuwa Kijana jasiri NA SHUJAA. KWANGU NAAMINI UJAFA BADO BALI WAISHI. KWANI SHUJAA HUWA HAFI BALI ANAPUMZIKA TU.

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...