Mineral occurrence in Tanzania by TMAA |
UONGEZAJI WA PATO LA MTANZANIA
Mheshimiwa Spika,
46. Lengo la Dira ya
Taifa ya Maendeleo ni kuiwezesha Tanzania kuwa na Uchumi wa Kipato cha Kati
(Middle Income Country) ifikapo mwaka 2025. Kwa mujibu wa Takwimu za Taasisi ya
Taifa ya Takwimu (National Bureau of Statistics) za mwaka 2010; wastani wa
Kipato cha Mtanzania kimefikia Dola za Kimarekani 545, sawa na Shilingi 770,464. Hivyo, katika kipindi
cha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka 15 tunayo changamoto
kubwa ya kuongeza kwa kasi kubwa Kipato cha Mtanzania ili kufikia lengo
lililokusudiwa la kufikia Dola za Kimarekani 3,000 ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 4.8 kwa mwaka au
Shilingi 400,000/= kwa mwezi ifikapo mwaka 2025 na hivyo kuifanya Tanzania kuwa
Nchi ya Uchumi wa Kati.
Mheshimiwa Spika,
47. Napenda kutumia
fursa hii kueleza kidogo kuhusu mwenendo wa takwimu za Mikoa kuhusu kiashiria
hiki cha Wastani wa Kipato cha Mwananchi (Regional Per-Capita Income).
Mtiririko wa nafasi za Mikoa kwa mwaka 2010 za Wastani wa Kipato cha Mwananchi
kwa mwaka ni kama ifuatavyo:
i. Dar es Salaam -
Shilingi 1,740,947
ii. Iringa -
Shilingi 979,882
iii. Arusha -
Shilingi 945,437
iv. Mbeya -
Shilingi 892,877
v. Kilimanjaro -
Shilingi 879,432
vi. Ruvuma -
Shilingi 866,191
vii. Mwanza -
Shilingi 829,647
viii. Manyara -
Shilingi 772,364
ix. Tanga -
Shilingi 763,203
x. Morogoro -
Shilingi 744,234
xi. Rukwa -
Shilingi 726,658
xii. Mtwara -
Shilingi 700,436
xiii. Lindi -
Shilingi 673,096
xiv. Mara -
Shilingi 642,528
xv. Pwani -
Shilingi 572,466
xvi. Tabora -
Shilingi 528,832
xvii. Shinyanga -
Shilingi 510,023
xviii. Kigoma -
Shilingi 499,428
xix. Kagera -
Shilingi 491,713
xx. Dodoma -
Shilingi 485,211
xxi. Singida - Shilingi 483,922
Mheshimiwa Spika,
48. Takwimu hizo zinaonesha kuwa Theluthi Moja
tu ya Mikoa yote ya Tanzania ndiyo yenye Wastani wa Pato la Mtu ambalo ni juu
ya Wastani wa Pato la Mwananchi Kitaifa la mwaka 2010 la Shilingi 770,464.
Vilevile, Takwimu hizo zinaonesha kuwa Mikoa Mitano ya mwisho kwa mlinganisho
wa Wastani wa Kipato cha Mwananchi ni Shinyanga,
Kigoma, Kagera, Dodoma na Singida. Hata hivyo, hali halisi inaonesha kuwa
Mikoa hii ina fursa nyingi za kuongeza Mapato kutokana na shughuli mbalimbali
za uchumi, na fursa za kibiashara zilizoko lakini Takwimu za Mapato ya Mikoa
hii haziwiani na hali halisi za maisha ya Wananchi wa Mikoa husika kwa fursa
walizonazo. Mikoa niliyoitaja ndiyo inaongoza kwa eneo kubwa la Ardhi nzuri na
idadi kubwa ya Mifugo Nchini ambayo pia ina fursa kubwa ya kuwaongezea Mapato.
Pia Mikoa hii ina idadi kubwa ya Wananchi wanaojishughulisha na Kilimo cha
Mazao yenye tija kubwa kama vile Pamba, Karanga, Alizeti na Ufuta. Aidha,
biashara imeshamiri sana kwenye Mikoa hii, hivyo hakuna sababu ya Mikoa hii
kuwa nyuma katika kipato cha Mwananchi. Vilevile, Mikoa mingine yote inayo
fursa tele za kuwaongezea Wananchi wake Kipato na kupunguza Umaskini.
From: PM Mizengo Pinda speech of August 26, 2011
Takwimu hizi zaonesha ama kuashiria nini? kama hali ndo hii kwanini watu woote wasikimbilie Dar? maana ndo kwenye unafuu ati! wewe wasemaje? toa maoni yako tafadhari.
No comments:
Post a Comment