April 16, 2010

NEC yatangaza majimbo mapya na ratiba ya uchaguzi 2010

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

“TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UGAWAJI WA MAJIMBO NA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU WA 2010”

1.Ugawaji wa Majimbo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ,Kwa mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,inawatangazia wadau wa Uchaguzi na Wananchi kwa ujumla kuwa itagawa Majimbo ya Uchaguzi yafuatayo.

i.Nkasi

ii.Tunduru

iii.Maswa

iv.Kasulu Mashariki

v.Bukombe

vi.Singida Kusini

vii.Ukonga

Taarifa zaidi kuhusu Majimbo hayo mapya yatakayoanzishwa itatolewa baada ya Tume kukutana na wadau wa Majimbo husika.

2. Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 Kwa mujibu wa Vifungu vya 37(1)(a) na 46(1) vya Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Vifungu vya 41(1) na 48(1) vya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ,Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia inawatangazia Wananchi wote kuwa Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 kwa Uchaguzi wa Rais, Bunge na Madiwani itakuwa kama ifuatavyo;

1. UTEUZI WA WAGOMBEA - 19 AGOSTI,2010

2, KAMPENI ZA UCHAGUZI -20 AGOSTI, HADI 30 OKTOBA,2010

3. UPIGAJI KURA 31 OKTOBA, 2010

Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi, Tume itawatangazia Wananchi rasmi, tarehe ya kutoa Fomu za Uteuzi kwa wagombea.

JAJI MSTAAFU LEWIS M.MAKAME MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...