May 21, 2009

Mwakyembe alazwa MOI.

Dr H Mwakyembe akishushwa toka ktk ndege ya kukodi na kupelekwa moja kwa moja MOI kwa Matibabu zaidi, 
Dr Mwakyembe alipata ajali ya gari mapema leo asubui huko mkoani Iringa akielekea Dar toka kuwaona wapiga kula wake.
Mungu akujalie upone haraka. 

3 comments:

Anonymous said...

francisgodwin.blogspot.com anathibitisha baadhi yaliyozungumzwa katika ripoti hii.Lakini inasikitisha kwamba Francis Godwin, ambae iaelekea alikuwa Iringa wakati wa kuandika,hakumhoji dereva na alizungumza na wengine tu (wengine ambao hata majina hayajatajwa) kabla ya kuandika story yake.

Francis Godwin anasema ni matairi mawili ya mbele na si moja tu yaliochomoka- hali isiyo ya kawaida.Lakini Francis Godwin alishindwa kupiga picha ya gari sehemu ya matairi mawili ya mbele kutuonyesha jinsi yalivyochomoka.Kama yalichomokea sehemu za kufunga nati basi inawezekana ya yalilegezwa usiku pale Makambako maana gari ilisafiri vizuri tu kutoka Kyela mpaka Makambako.Hata kama yalichomokea kwenye tie rods inawezekana zililegezwa usiku pale Makambako.

Alafu Francis Godwin alishindwa kutupatia jina la hoteli aliyolala mbunge pale Makambako. Aidha ameshindwa kumhoji hata mtu mmoja kwenye hoteli hiyo.Hii ni muhimu maana kuna tetesi kwamba kuna watu wasiojulikana walikuwa wakifuatilia gari ya Mbunge kutoka Kyela.

Alafu shimo ambalo Francis Godwin anadai lilisababisha ajali ni dogo mno (linaonyeshwa kwenye link iliyotajwa hapo juu). Francis anasema dereva aliingiza gari katika shimo wakati anaovateki lori.Lakini taarifa zingine zinasema kwamba dereva alikuwa akihangaika kucontrol gari baada ya gari kuanza kuyumba alipoingia kwenye bara bara kuu na kuanza kuchukua kasi katika safari ya kwenda Dar kutoka Makambako.Katika kuhangaika huko gari iligongana na hiyo lori ubavuni na kisha kuhama barabarani.

Anonymous said...

Hiyo lori iliigonga gari ya mbunge wakati gari ya mbunge ikimalizia kuipita lori.Dereva wa lori alikuwa akiizuiazuia gari ya mbunge ispite, lakini mwishowe akairuhusu,ilipofika katikati akaanza kubana upande wa gari ya mbunge.Hali amabayo ilimfanya dereva wa mbunge aongeze moto/spidi ili apite kwa haraka, alipokuwa akiimalizia kuovertake lori ikabetua gari ya mbunge kwenye kona kwa nyuma.Gari ya mbunge ikakosa mwelekeo pamoja na jitihada za dereva kuirudisha barabarani,ikatoka nje ya barabara kupinduka mara kadhaa porini. Lori haikusimama bali iliongeza moto ikielekea Dar.Kuna wasafiri waliotokea upande wa Iringa/Dar waliothibitisha kupishana na lori iliyokuwa ikitembea kwa mwendo wa kasi ajabu kabla hawajafikia eneo la ajali ilipokuwa gari ya mbunge- somma Tanzania Daima ya leo. Hii jamani ajali au mipango??Waandishi wa habari wa Tanzania nawaomba na nawsihi acheni kuandika anayotaka bosi au mwenye mali.Nendeni mkachunguze mazingira ya kugongwa Dk Mwakyembe- hapo ndipo mtaelewa ushujaa wa mbunge wenu huyu na mamabo yalivyo nchini na mafisadi wako tayari kufanya nini kuung'ang'ania uchumi wa TZ.
Tunamshukuru Mungu kwa kumnusuru Mbunge wetu, tunamshukuru kwa teknohama hii inayotuwezesha kutoa taarifa kwa faida ya watanzania wenzetu bila woga, tunamuomba aendelee kuwalinda viongozi wetu wote watakaotuondoa katika makucha ya ufisadi na unyonyaji,tunamuomba atupe na sisi wananchi ujasiri wa kufuata ukweli na kuwafuata viongozi wapinga ufisadi.

Yasinta Ngonyani said...

Pole sana na Tanzania na pole sana wanafamilia

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...