MFANYABIASHARA maarufu nchini, Idd Simba, amesema, lugha ya kiingereza imesababisha Tanzania iwe na sheria mbaya zikiwemo za madini.
Mbunge huyo wa zamani wa Ilala, Dar es Salaam, amesema, anaona aibu kwa kuwa alishiriki kupitisha sheria mbaya za madini zinazotumika kuinyonya nchi.
Mwanasiasa huyo amedai kuwa, chanzo cha ubaya wa sheria hizo ni lugha ya kiingereza kwa kuwa sheria zimeandikwa kwa lugha hiyo lakini idadi kubwa ya wabunge hawaielewi kwa ufasaha.
“Zile sheria ni mbaya na mimi naona aibu kwamba zilipitishwa wakati nikiwa kwenye lile Bunge, lakini unatarajia nini wakati sheria zile zinatungwa kwa Kiingereza, na si wabunge wengi wanaoelewa lugha hiyo,” amesema.
No comments:
Post a Comment