TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Nimesikitishwa na kufedhesheshwa na taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa Iringa Jumatatu iliyopita na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini James Kombe na kutangazwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu mazingira ya ajali ya gari niliyopata tarehe 21, Mei 2009, saa 1 na dakika 10 eneo la Ifunda, mkoani Iringa. Taarifa hiyo ya Polisi inakanusha maelezo yangu yote na ya dereva wangu kuhusu ajali ilivyotokea na kunitaka nijiepushe kutoa matamshi kuhusiana na ajali hiyo kwa madai kwamba sina utaalamu na masuala ya ajali. Taarifa hiyo nimeipata kupitia gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 26, 2009 na kwa kuwa uwasilishwaji wake haujalalamikiwa na Jeshi la Polisi, naichukulia taarifa hiyo kuwa sahihi.
Pamoja na kwamba bado naumwa na niko nyumbani nikipumzika kwa ushauri wa madaktari, nimelazimika kuvunja ukimya na kutoa taarifa hii fupi kuzuia upotoshaji wa makusudi unaofanywa na magazeti, hususan gazeti la Tanzania Daima, na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi kwa sababu wanazozijua wenyewe kuhusu suala hili. Aidha nataka kuelezea masikitiko yangu kuhusu hatua hiyo ya Jeshi la Polisi ambayo ina mwelekeo zaidi wa kisiasa kuliko utaalamu wa upelelezi na uendeshaji mashitaka kama ifuatavyo:
No comments:
Post a Comment