Rais JK jana alielekea Kenya kujaribu kuokoa mazungumzo ya upatanishi kati ya ODM na Serikali ya Mwai Kibaki ambayo mpatanishi wake Kofi Annan alitangaza kuwa YAMEKWAMA JANA.
Raila Odinga leo hii ametangaza kusitisha maandamano aliyokuwa ameyaita kufuatia ushauri wa Mpatanishi Kofi Annan,
Ndugu zetu wakenya ebu kaeni ktk meza ya mazungumzo jaribuni kaafikiana ili kumaliza mgogoro huu kwani wanaoteseka ni raia wadogo na zaidi kinamama na watoto na si nyie wanasiasa ambao mnauwezo wa kuruka wakati wowote kwenda kokote mtakako,
jaribuni sana kuwafikilia hawa wadogo wanaoteseka legezeni misimamo yenu kwa manufaa ya wakenya wote, misimamo mikali haitasaidia ktk hali tete kama hii.
Thaminini mchango mkubwa wa wapatanishi hawa Kina Annan, Graca Machel, Ben Mkapa ambao hata kama ni wastaafu lakini wanazashghuri muhimu za kufanya ila wameziacha na kukaa nanyi kujaribu kutafuta suruhu ya jambo hili, pia michango ya viongozi mbalimbali akiwemo rais Kikwete ambaye yasemekana alilazimika kumwomba Rais wa Uturuki na ujumbe wake kuahirisha ziara na kwenda moja kwa moja Kenya kujaribu kuokoa jahazi la upatanishi.
VIONGOZI WA ODM NA SERIKALI YA KIBAKI JUKUMU LA AMANI, USTAWI NA MUSTAKABALI WA KENYA LIKO MIKONONI MWENU.
No comments:
Post a Comment