DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT¢S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ziara ya Rais wa Uturuki yaahirishwa
Na mwandishi maalum,
`Ziara ya Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Abdullah Gul katika Tanzania, iliyokuwa ianze leo, imeahirishwa..
Rais Gul alitarajiwa kuwasili nchini leo, kwa ziara rasmi ya siku mbili kwa mwaliko wa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Gul alitarajiwa kuwasili nchini na kundi kubwa la wafanyabiashara wapatao 160 kutoka Uturuki.
Wakati wa ziara yake, mbali na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Kikwete, Rais Gul pia alitarajiwa kuhutubia mkutano wa pamoja wa wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki.
Tanzania na Uturuki pia zilitarajiwa kutia saini mkataba wa ushirikiano wa kiufundi, kisayansi na kiuchumi katika eneo la kilimo.
Imetolewa Na
Bw. Salvator Rweyemamu,
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Habari,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Februari, 2008
No comments:
Post a Comment