Mpaka jana usiku mchuano mkali ulikuwa kati ya CCM na CHADEMA huku CUF na vyama vingine vikifuatia kwa mbaali kwa mujibu wa matangazo yaliyokuwa yakirishwa moja kwa moja na ITV na Radio One.
Mitandaoo mbalimbali imekuwa kitoa ubashiri wao ama matokeo yasiyo rasmi, wapo waliosema kuwa CCM imeshinda huku wengine wakisema CHADEMA imeshinda, CUF iliyokuwa ikidai kuwa ina mtaji wa kura zaidi ya 10,000 zinaonekana kuyeyuka, je ni nini kimeyeyusha kura zao miezi 11 tu baada ya uchaguzi ule? bila shaka kuna somo hapo.
Matokeo rasmi tunayatarajia muda wowote kwani watu wamekesha pale ofisi ya halmashauri ya Igunga kusubiri ujumlishaji wa matokeo toka kwenye vituo mbalimbali.
Kwa mijubu wa Tume ya Uchaguzi watu waliojiandikisha na hivyo kuwa na sifa ya kupiga kura ni 174, 077 lakini kwa mujibu wa matokeo yanavyopokelewa na kuripotiwa kuna hati hati ya wapiga kura kufika ama kukaribia nusu ya wapiga kura wote halali, je hii inasababishwa na nini? kwanini watu zaidi ya nusu hawajajitokeza kupiga kura? je kuna walakini katika Daftari la Kudumu la wapiga kura? Itakumbukwa kuwa Uchaguzi mkuu uliopita ulikuwa na tatizo hili pia.
No comments:
Post a Comment