Nimeshtushwa sana
na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi
kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata
Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea
mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.
Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao
bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na
mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni
tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama
nafasi ya kujitajirisha binafsi.
Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi
wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za
vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati
wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati
Kuu ya chama kujadili suala hili.
Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za
vikao. Popote ninapohudhuria vikao
huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba
wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona
kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa
kabisa wamechukua posho.
Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu.
Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la
posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?
Tazama nchi hii,
juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati
wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.
Tanzania inaagiza
gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za
kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek
Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na
marupurupu mengine.
Ipo siku
Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao.
Zitto Kabwe(MB)
Kigoma Kaskazini -Chadema
No comments:
Post a Comment