Nipashe: LOWASSA AJIELEZA NEC
Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
imemaliza kikao chake jana huku aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa,
akisimama na kutoa dukuduku lake
kuhusiana na tuhuma za
ufisadi dhidi yake.
Kikao hicho cha siku mbili kilichoketi chini ya Mwenyekiti
wake Rais Jakaya Kikwete, ambacho kilimalizika jana saa 11:30 jioni, mtoa
habari wetu alikuwa ndani ya kikao hicho alisema Lowassa, alisimama na kueleza
masikitiko yake juu dhana ya kujivua gamba ilivyoendeshwa wakati kikao hicho
kikijadili hali ya siasa nchini.
Chanzo chetu kilimkariri Lowassa akisema kama ni suala la
kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond ,
alitaka kuuvunja mkataba kati ya kampuni hiyo na Shirika la Umeme nchini
(Tanesco) mapema, lakini Rais Kikwete aliyekuwa nje ya nchi alikataa kufanya
hivyo na badala yake alimwambia kuwa anasubiri ushauri wa makatibu wakuu wa
wizara.
Alisema aliamua kujiuzulu nafasi zake katika serikali ili
kulinda heshima ya serikali na chama chake, lakini anashangazwa na hatua ya
wanaCCM wenzake na si wapinzani kuzunguka mikoani kumchafua wakidai kuwa yeye
ni fisadi.
Lowassa alimkumbusha Mwenyekiti kuwa kumekuwa na utamaduni
wa kupikiana majungu ndani ya chama na kukumbushia tukio la yeye (Kikwete)
kuzushiwa mengi na Daud Mwakawago wakati wa harakati za kuusaka urais kabla ya
2005.
“Mwenyekiti wewe unakumbuka wakati Mwakawago alipokuja na
rundo la tuhuma za hisia, isingekuwa busara za Rais Mkapa (Rais wa awamu ya
tatu, Benjamin Mkapa), wewe usingekuwa hapo ulipo,” chanzo hicho kilimkariri
Lowassa akisema.
THE National Executive Committee of the Ruling Party, Chama
Cha Mapinduzi (NEC-CCM), on Thursday ended its two-day meeting without
expelling or stripping some prominent cadres of their posts as speculated
earlier.
However, the Dar es Salaam Regional Party Secretary, Kilumbe
Ng'enda, was relieved of his duties.
The party's Ideology and Publicity Secretary, Mr Nape
Nnauye, promised reporters here on Thursday that he would address a press
conference on Friday.
Sources from the meeting however told the 'Daily News' that
the meeting resolved to forward the 'cleansing and skin shedding' business to
the Ethics and Security Committee, and the Central Committee (CC-CCM).
"The meeting decided that any CCM member who has
evidence of wrong-doing by the cadres should submit it to the two committees
for appropriate action," revealed the source.
Another high-profile NEC member said the meeting resolved to
'cleanse' the party without breaking it up.
"NEC members debated the philosophy, it was decided it
should be conducted with sobriety and with evidences," revealed another
NEC member.
MAWAZIRI Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick
Sumaye, jana walishambulia kwa maneno makali wajumbe wawili wa Sekretarieti ya
CCM kwamba wamekuwa wakikivuruga chama na kusababisha mgawanyiko uliopo.Lowassa
aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, kutokana na kashfa ya Richmond ndiye aliyekuwa wa
kwanza kuzungumzia suala hilo wakati wa mjadala wa hali ya siasa, katika kikao
cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichomazika jana mjini Dodoma.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema
Lowassa alianza kubwaga moyo wake baada ya NEC kuridhia ombi la Kamati Kuu ya
chama hicho (CC) kwamba suala la mageuzi ndani ya CCM maarufu kama
kujivua gamba lirejeshwe katika kamati hiyo ili lifanyiwe kazi kwa taratibu za
kawaida za kinidhamu baada ya wahusika kukataa kuachia nafasi zao.
“Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo
hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba
nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama
wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,”Lowassa
alinukuliwa akihoji.
Lowassa alinukuliwa akiwataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John
Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lowassa alitumia dakika saba
kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba
mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga.
Baada ya maneno ya Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali
ya Awamu ya Tatu, Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia
ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao.
“Mwenyekiti huyu bwana (Lowassa) amesema kwamba amechafuliwa
kwa miezi saba, sasa kama leo tunasema kwamba tunarudi kwenye utaratibu wa
kamati za maadili, hao waliomchafua watafanywaje?”Sumaye alinukuliwa akihoji.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya kikao hicho zilimnukuu
Kikwete akisema kwamba viongozi hao watakuchukuliwa hatua za kinidhamu kama
watakuwa wamefanya hivyo.
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete aliwasihi wajumbe kuachana na suala hilo na badala yake kuchangia
maeneo mengine ya taarifa hiyo ya hali ya siasa iliyowasilishwa na Katibu wa
Siasa na Mambo ya Nje ya CCM, January Makamba.
No comments:
Post a Comment