YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA
AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR .
Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa
na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na
wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa
ikitoka Unguja kuelekea Pemba .
Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa
inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.
Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya
maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko
mkubwa sana juu ya tukio hilo .
kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa
kuzingatia mambo yafuatayo:-
• Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na
nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya
Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .
• Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya
Yanga na Ruvu Shooting.
• Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za
muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.
• Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu
kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya
kupoteza nafasi hiyo
• Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani
lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.
Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika
maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini
walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa
kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao
ikiashilia maombolezo.
Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na
mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.
Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa
hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe
kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo
kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.
KUOMBA RADHI
Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi
na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi
wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu
wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na
Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA
HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza “TUNAOMBA
RADHI”
Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,
Amina,
Hashim Lundenga
Mkurugenzi
No comments:
Post a Comment