September 13, 2011

Hii inasikitisha sana, Familia nzima kuteketea na usijue waliko!!


Tulikuwa watu 36 wakubwa kwa watoto lakini walionusurika ni wanne tu, 32 wote wamefariki dunia katika ajali hiyo na kati ya watu waliofariki miili iliyoonekana ni saba waliobaki hawajaonekana mpaka sasa,” alisema Ally na kuongeza:
“Ingawa mimi ni mzima lakini mpaka hivi sasa sijui pakuanzia wala pa kutokea baada ya kutoka hospitali kwa sababu familia nzima imeteketea katika ajali hiyo.”Tulikusanyika wote tukasali 
“Kwa kweli nilipoona hivyo nikajua sasa tumekwisha. Nikarudi tena chini nikakuta maji yameshajaa ndani ya meli ndipo tukakusanyika wanandugu wote tuliokuwa ndani ya meli pamoja na maharusi wetu tukaswali swala ya mwisho na kuambizana kuwa kila mtu ajiokoe mwenyewe na Mungu akipenda tutakutana popote pale iwe duniani ama peponi,” alisema Ally.
“Niliwakusanya watoto wote baada ya kuona wazazi wao wamechanganyikiwa na ukizingatia kwamba hawana uzoefu na masuala ya maji nikawapa godoro na kuwaambia kwamba walishikilie kwani ndilo itakalowaokoa.”
“Baada ya kuwapa watoto godoro, nikarudi kuwatafuta ndugu wengine lakini sikufanikiwa kuwaona tena ndipo nilipoamua kurudi juu kutafuta jaketi nikapata moja nikalivaa kisha nikarudi nilipowaacha watoto na kuungana nao. Wakati huo maji yalikuwa yameshajaa ndani ya meli."
“Kidogo nikaokota mbao ambayo baadaye ilinisaidia kuvunjia moja ya dirisha la meli hiyo kwani wakati huo hata mlango ulikuwa hauonekani nikawapitisha watoto pamoja na mimi mwenyewe nikapita.”
“Nilipofika nje ya meli, nikakuta watu wengi wanaelea na majaketi yao wengine wakiwa wameshafariki dunia, kwa sababu yale majaketi kama hujui kuogelea hayawezi kukusaidia, isipokuwa ukifa huwezi kuzama badala yake utakuwa ukielea juu ya maji. Kadri muda ulivyozidi niliona watoto wakizidiwa na kuishiwa nguvu na mwishoni wote wakafariki dunia mbele yangu.”
Muda wote akisimulia, Ally alikuwa akibubujikwa machozi... “Baada ya kuona ndugu zangu wote wameteketea, ndipo nilipoanza kujiokoa mwenyewe na ilipofika saa 5:00 asubuhi, nikaona helikopta ikipita nikaanza kupeperusha shati langu kila wakati mpaka waliponiona na kuja kuniokoa.”
“Walipofika wakashusha kamba nikajitahidi kujivisha kwa shida kwani wakati huo wote hakuna hata kiungo changu kimoja kilichokuwa kinafanya kazi mwili ulianza kuchanika kwa sababu ya chumvi na baridi kali.”
Miongoni mwa walionusika alikuwamo mtoto wa miaka sita akiwa na dada yake mwenye umri wa miaka 12. Mama mdogo wa mtoto huyo, Mariam Hemedi alisema Said anaendelea vizuri na dada yake amesharuhusiwa kutoka hospitali.

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...