Bunge limepitisha kwa kauli moja marekebisho ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya Mwaka 2010, baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, kuwasilisha bungeni muswada wa sheria unaopendekeza marekebisho ya sheria 16, ikiwamo sheria hiyo.
Hatua hiyo ilifikiwa jana na Bunge, zikiwa zimepita wiki chache tangu Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, kukaririwa na vyombo vya habari akilalamikia kitendo cha serikali kuingiza vifungu ndani ya sheria hiyo kinyemela.
Vifungu vilivyolalamikiwa na Dk. Slaa kwamba, viliingizwa katika sheria hiyo nje ya utaratibu wa Bunge, ni pamoja na vifungu vidogo vya 1, 2 na 3.
Dk. Slaa, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema, alisema vifungu hivyo viliingizwa katika Kifungu cha 7 baada ya sheria hiyo kujadiliwa na kupitishwa na Bunge, kitu ambacho ni kinyume na utaratibu.
Kutokana na
swali!!
Wadau je kuingiza vifungu kinyemela na baadaye kushtukiwa lakini pamoja na kushtukiwa huko wakana na sasa waamua kuondoa vifungu ama kurekebisha tu kwatosha? hakuna makosa mahali fulani hapo? Je Mkuu wa Nchi hakudanganywa ama kuuziwa mbuzi kwenye gunia?
source:Nipashe
No comments:
Post a Comment