Mwasisi wa habari za jamii mtandaoni (social media) Bw. Muhidin Issa Michuzi anaondoka leo kuelekea London, Uingereza, kuhudhuria kongamano la pili la Watanzania wanaoishi nchi za nje (Diaspora 2 conference) kwa mwaliko maalumu akiwa kama blogger.
Bw. Michuzi, ambaye ametoa mchango mkubwa katika kupromoti habari za jamii mtandaoni kupitia blog yake maarufu ndani na nje ya nchi iitwayoissamichuzi.blogspot.com, amealikwa huko mkutanoni na ubalozi wetu Uingereza ili kutoa mada inayohusu umuhimu wa habari za jamii mtandaoni katika kujenga daraja kwa walio ndani na nje ya nchi.
Bongo Pix yakutakia kila la kheri. Bravooo.
No comments:
Post a Comment