Kuanza na hatimaye kuumaliza mwaka ni neema ya MUNGU, hakika sisi binadamu hatuna cha kujivunia hapo, sote twajua na hata mzee wetu Simba wa Vita alipenda bila shaka kuuona mwaka 2010 lakini Bwana amempenda zaidi na hivyo amemuita kwake siku ya mwisho kabisa ya mwaka.
Kwa namna ya pekee napenda kuchuka nafasi hii kuwashukuru wadau wote ambao mmesafiri nami katika blogu kwa mwaka 2009, kabla ya kuwatakia heri ya mwaka mpya naomba kwanza kuwaomba msamaha wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine niliwakosea ama kuwakwaza ktk jambo lolote lile, sisi ni binadamu na katika ubinadamu wetu hatukukamilika hivyo kukwaruzana hapa na pale ni vitu vya kawaida kabisa kwa kujua ama kutojua, jambo la msingi mara utambuapo umemkwaza mtu basi ni kuomba msamaha, nami pia nawasamehe wote ambao walinikwaza na zaidi na waombea pia.
KWA UPENDO MKUU NAWATAKIA WASOMAJI WANGU WOOOOOOTE HERI YA MWAKA MPYA WA NEEMA NA MAFANIKIO WA 2010,
Naomba kuwapa neno hili la kinabii toka kwa Nabii wa Mungu Isaya lituongoze mwwaka huu 2010. Naamini Neno hili litafanyika baraka kwetu sote bila kujali dhehebu au dini.
1 "Arise, shine, for your light has come,
and the glory of the LORD rises upon you.
2 See, darkness covers the earth and thick darkness is over the peoples, but the LORD rises upon you and his glory appears over you.
Isaiah 60:1-22
No comments:
Post a Comment