Pichani ni Rais wa Afrika Kusini,Jacob Zuma,akicheza ngoma ya asili ya ki-Zulu na mkewe mpya,Thobeka Madiba,katika harusi yao iliyofungwa huko kijijini kwao katika jimbo la KwaZulu.
Kuna mtu kauliza,mbona kuna watanzania wanamshambulia Rais Zuma kwa kuwa na wake watatu?Mbona Rais wetu mstaafu alikuwa na wake wawili?
Picha ya AFP
1 comment:
Mwacheni Zuma "afaudu maisha". Anadumisha mila na utamaduni wa Mwafrika huyu. Kuna nini cha kushangaza hapa? Waisilamu tukioa wake wengi mbona hamtushangai?
Kule Usukumani (na naamini pia katika makabila mengi) bado ni rukhsa kuoa wake wengi na kijijini kwetu kuna jamaa wenye wake wawili, watatu, wanne, watano na hata sita.
Hata hao wasio na wake wengi - wana nyumba ndogo Ilala, Temeke na Kinondoni? Si ni kitu kile kile tu au?
Post a Comment