August 8, 2009

Nini kinaendelea CCM,

KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amepinga kauli ya makamu mwenyekiti wa zamani, John Malecela kwamba, chama hicho kitakuwa na wakati mgumu katika Uchaguzi Mkuu ujao. Juzi Malecela alisema CCM itakuwa na wakati mgumu katika uchaguzi huo wa mwaka 2010 kwa sababu ya tuhumu nyingi za ufisadi na baadhi ya wabunge wake kushindwa kutekeleza ilani ya chama hicho ya mwaka 2005.
Kwa mujibu wa Malecela, vita dhidi ya mafisadi ni ngumu kwa sababu ndani ya CCM kuna baadhi ya watu wanaokichafua chama kwa tabia zao za kuungana na mafisadi. Lakini, Makamba jana alisema ufisadi anaozungumzia Malecela kwamba utakisambaratisha chama hicho mwakani ni wa kufikirika kwa sababu mpaka sasa hakuna mwenye ushahidi unaodhihirisha kwamba fulani ni fisadi.
"Mimi siwajui hawa mafisadi. Hebu wewe nitajie jina la mtu mmoja ambaye una ushahidi kuwa ni fisadi," alisema Makamba.
Alipoulizwa kuhusu baadhi ya makundi ya mafisadi ambayo tayari yameanza kampeni ya kusambaza pesa za kuwaangusha kwenye majimbo wabunge walio mstari wa mbele katika vita dhidi yao, Makamba alisema, "siyo kweli ila ni jambo ambalo linakuzwa tu."

1 comment:

Anonymous said...

hello... hapi blogging... have a nice day! just visiting here....

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...