Wema akibebwa msomsobe na Mama yake baada ya kutaka kuondoka na "mumewe" Jumbe ambaye familia yake haimtambui.
"Nakwambie twende nyumbani haraka kama sivyo ninakufutia dhamana yako sasa hivi ili urudishwe rumande haraka huyo Jumbe si hatumtambui na kama anakupenda mbona hajakudhamini?” Mama Wema.
“ Mimi labda nife ndio mwanangu ataolewa na kijana huyo sitaki hata kumuona kwa kuwa kwanza ndio chanzo cha mwanangu kuharibika, lakini hata hivyo mimi naona kama alikuwa na nia na mwanangu mbona hata dhamana hakuja kumtolea dhamana” aliendelea kufoka Mama kwa hasira.
MISS Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu jana aliachiwa kwa dhamana katika kesi inayomkabili ya kuvunja kioo cha gari cha Msanii Stephen Kanumba chenye thamani ya Shilingi milioni moja.
No comments:
Post a Comment