Mwandishi wa habari wa Magazeti ya Mwananchi katika kituo cha Dodoma Michael Uledi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mirembe alipokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Uledi ameacha mke na mtoto mmoja na taratibu za mazishi zinafanyika kwa kushirikiana kati ya kampuni la Mwananchi na ndugu wa marehemu nyumbani kwa Marehemu Nkuhungu mjini Dodoma, mwili wa marehemu unatarajia kusafirishwa leo kwenda Kijijii kwao Buigiri Kilomita 35 kutoka Dodoma mjini ambako mazishi yatafanyika kesho saa 5 asubuhi
No comments:
Post a Comment