May 27, 2008

CHEE NKAPA AZOZA

RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amevunja ukimya kuhusu tetesi na tuhuma kwamba alikiuka misingi na kujikita katika biashara wakati akiwa madarakani kwa kusema madai hayo si ya kweli na kwamba wanaomtuhumu wana chuki dhidi yake. Akihutubia mwishoni mwa wiki katika Kijiji alichozaliwa cha Lupaso, Wilaya ya Masasi, Mkapa alisema wanaomtuhumu wanamchukia kwa kutowapendelea wakati wa utawala wake. Katika hotuba yake hiyo aliyoitoa wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kwa Kituo cha Afya kinachomilikiwa na Kanisa la Katoliki kijijini hapo, alisema; “Msisikilize uongo huo kwa sababu hauna msingi wowote isipokuwa ni chuki …hasa inayotokana na watu ambao walifikiri nitawapendelea … sikuwapendelea,” alisema Mkapa huku akishangiliwa na wanakijiji wenzake waliohudhuria makabidhiano hayo. Alisema kuwa yeye si tajiri na kwamba tuhuma hizo ni za uongo na hivyo kuwataka wananchi kuzipuuza kwa kuwa hazina msingi wowote wala chembe ya ukweli. “Sina uwezo wa fedha ingawa najua mnasikia na kusoma mengi …naishi kwa pensheni yangu kutoka serikalini kutokana na kuwa kiongozi kwa miaka 10 ambayo hata Mzee Mwinyi anaishi hivyo maana sisi sote ni wastaafu. Huo (uvumi) ni uongo …uongo ….uongo ….uongo …uongo….uongo….uongo,” alisema Mkapa na kuongeza; “Mimi si tajiri, nimeomba msaada nimepewa…nimejinyima mimi na mke wangu ndiyo tukaweza kugharimia kusafirisha vifaa hivi kutoka Canada hadi Dar es Salaam, kutoka hapo hadi hapa vimesafirishwa na Serikali…..sikuwa na uwezo wa kununua vifaa kama hivi. Nitapata wapi fedha za kununua vifaa kama hivi,” alisema Mkapa.
Posted by Picasa

1 comment:

Anonymous said...

Ebwana unatudanganya katika hiyo picha yako ya hapo pembeni. hivi unaweza kweli kupiga picha hapo ilhali jicho la kushoto lipo wazi?
Nipe jibu.

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...