HALI ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan,
ilibadilika ghafla jana jioni kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.Zitto alilazwa Aga Khan juzi jioni baada ya kusumbuliwa na maumivu ya
kichwa kabla ya kuruhusiwa na kisha kurudishwa baada ya maumivu hayo kuendelea.
Kaka wa mbunge huyo, Salum Mohamed alisema jana jioni kwamba
hali ya mdogo wake ilikuwa ikiendelea vyema lakini ilibadilika ghafla na kuanza
kutetemeka.
“Hali yake ya Zitto imegeuka kuwa mbaya, anatetemeka mwili
mzima na sasa tunampeleka Muhimbili kwa uangalizi zaidi,” alisema Mohamed.
Jana jioni, mwandishi wa gazeti hili alimtembelea Zitto Aga
Khan jana majira ya saa kumi jioni na kumkuta akiwa anaendelea vyema. Zitto,
ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alisema
maeneo mengine katika mwili wake yalikuwa yamepona isipokuwa maumivu ya kichwa.
Awali, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema,
Erasto Tumbo alisema Zitto anasumbuliwa na ugonjwa wa kipanda uso.
Aliwataka wanachama wake chama hicho, kumuombea kiongozi huyo
ili apate nafuu na kushiriki kikamilifu kwenye vikao vya Bunge vinavyotarajiwa
kuanza Oktoba 8, mwaka huu.
Source: Mwananchi.
No comments:
Post a Comment