Picha naYassin Nicas Mtei |
MIILI ya watu 12 walioteketea kwa moto katika ajali ya basi
la Deluxe Coach iliyotokea Misugusugu mkoani Pwani juzi, watazikwa leo na
Serikali kwa heshima zote katika kaburi moja katika eneo la Air Msae mjini
Kibaha.
Eneo hilo
ndipo walipozikwa watu waliopata ajali ya basi la Air Msae lililokuwa likitokea
Arusha kuja Dar es Salaam miaka ya 1990.
Uamuzi huo umefikiwa jana katika kikao cha Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa wa Pwani, iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mwantumu Mahiza
kutokana na miili hiyo kuharibika vibaya na kushindwa kutambulika.
Akizungumzia mazishi hayo jana, Mahiza alisema kabla ya
maziko, miili ya watu hao itachukuliwa sampuli kwa ajili ya vipimo vya vinasaba
(DNA) ili vifanikishe utambuzi wao.
Taarifa kutoka Hosptali Teule ya Tumbi, zilieleza kuwa hata
wananchi waliokwenda kujaribu kutambua ndugu zao, walishindwa kufanya hivyo
kutokana na kuharibika kwa miili hiyo ambayo baadhi imekuwa majivu.
Kutokana na hali hiyo, Mahiza aliwataka wananchi kutoa
ushirikiano katika kufanikisha kuwatambua ndugu zao, kwa kupeleka vitu kama nguo ambazo ndugu zao walizitumia siku chache kabla
ya ajali hiyo.
Habari Leo,
No comments:
Post a Comment