September 26, 2011

Shule za Kata hazifai!


Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa, amesema haungi mkono shule za sekondari za kata nchini kwa sababu hazijaandaliwa vizuri kuwawezesha watoto kukomaa na kupata elimu iliyo bora.

Aliyasema hayo jana katika mahubiri yake kwenye kanisa kuu la Anglikana Mbeya ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake ya kutembelea Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini ya kanisa hilo. Dk. Mokiwa alisema shule nyingi za kata zimejengwa kisiasa na ndiyo maana hata elimu inayotolewa katika shule hizo haikidhi mahitaji ya ushindani wa kielimu. 

Alisema kutokana na shule hizo kujengwa kwa manufaa ya kisiasa, wanafunzi wake wamekuwa wakisoma kwa mtindo wa kinadharia na kukaririshwa, alisema hali ambayo haimfanyi mwanafunzi kuelewa vizuri. “Vijana wa siku hizi mnafundishwa maswali yote mnapewa majibu ya kuchagua, mnapofundishwa suala la ufahamu mnashindwa kuelewa,” alisema Dk. Mokiwa.

 Askofu Dk. Mokiwa alisema ili kurudisha elimu katika kiwango bora, serikali irejeshe shule za  zilizokuwa zikimilikiwa na taasisi za dini ili wao waziendeleze kwa sababu shule hizo zilimjenga mwanafunzi kiroho na kiakili. 

Alisema serikali ilizichukua shule hizo  kama majengo na kuacha msingi ambao ulikuwa umewekwa na shule hizo ambao ulikuwa na mfumo mzuri wa ufundishaji uliozingatia maadili ya mwalimu na mwanafunzi. “Shule za misheni zirudi ni mali ya kanisa, na zitarudi zenyewe au kwa kurudishwa na waliozichukua,” alisisitiza Dk. Mokiwa. 

Akizungumzia suala la ufisadi, Dk. Mokiwa alisema ufisadi ni roho na tabia mbaya ambayo ipo katika kada mbalimbali kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa. 

Alisema ufisadi unapaswa kukemewa kuanzia ngazi ya familia kwani ikiachwa  baadaye unaharibu taifa katika sekta za bararabara na umeme na hivyo kuzua malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania.


SOURCE: NIPASHE

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...