September 10, 2011

Baa 12 zachomwa moto Zenji!!







Baa nyingine mbili zimechomwa moto katika mtaa wa Mbweni katika Mkoa wa Mjini Mgharibi mjini Zanzibar.Baa zilizochomwa moto usiku wa kuamkia jana ni Nyamachoma na Executive Park ambazo walioshuhudia walisema zilianza kuwaka moto kwa wakati moja saa 12:00 alfajiri.

Zaidi ya watu watano walinusurika kufa katika baa ya Executive ambayo upande mmoja ni nyumba ya kulala wageni.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo watu wenye silaha za kienyeji na bunduki walifyatua risasi hewani kuwatisha walinzi kabla ya kumwaga petroli katika majengo hayo na kuyalipua moto.

Baadhi ya wafanyakazi wa baa ya Executive walisema wakati wamelala walisikia watu wakipita nje na baadaye kidogo kuona jengo linawaka moto na kelele za kuwataka watoke nje.

“Tulipotoka nje, tayari moto ulikuwa umeshika jengo lakini watu walitupa taarifa ya kututaka kuamka nao tayari walikuwa wamekimbia,” alisema mfanyakazi mmoja wa baa hiyo.

Hata hivyo, alisema tukio hilo lilitokea baada ya watu wasiopungua wanne kumtishia mlinzi kwa bunduki na kufanikiwa kuchoma moto baa hiyo.

Meneja wa baa ya Nyamachoma, Muumini, alisema baa hiyo ilikuwa na walinzi wasiopungua wanne ambao ni vijana wa Kimasai.

Alisema wakati watu hao wanaivamia kila mmoja akiwa amevalia kanzu na koti, walinzi wa baa hiyo walikuwa wanaangalia televisheni ukumbini.

“Polisi wamefanikiwa kuokota mabaki ya baruti, inaonekana wahalifu wallikuwa na bunduki bandia iliyosababisha walinzi kusita kupambana nao,” alisema meneja huyo.Akiwashukuru waliosaidia kuzima moto huo, meneja huyo alisema juhudi hiyo ilifanikishwa na majirani kwa ushirikiano mkubwa na Kikosi cha Zimamoto.

Aliungana na wamiliki wengine wa baa kulalamikia kitendo cha Serikali ya Zanzibar na ya Muungano kushindwa kuchukua hatua za kupambana na uhalifu huo, ambao tayari umesababisha baa 12 kuchomwa moto tangu Januari, mwaka huu.

Hakuna mtu aliyekamatwa kutokana na uhalifu huo, lakini Kamishana wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, katika mahojiano na NIPASHE mara kadhaa alisema matukio hayo ni hujuma na kusema uchunguzi unaendelea.

Si Serikali ya Zanzibar wala ya Muungano zilizotoa tamko lolote juu ya matukio hayo.Viongozi wa Umoja wa Wamiliki wa Vileo Zanzibar wameomba msaada kupitia njia mbalibali.

Source: Nipashe

Kwa tukio hili inatimiza baa 12 zilizochomwa moto tangu mwezi Januari, hakuna aliyekamatwa wala kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, kwani pamoja na sababu zozote wanazoweza kuwa nazo wahuni hao, ndio ni wahuni (haiingii akilini mtu mwenye akili zake timamu kufanya hayo) dado kitengo hicho naamini ni cha jinai na inapaswa sheria kuchukua mkondo wake, je ni sababu gani hakuna aliyekamatwa, kuhojiwa au kufkishwa mahakamani? mamlaka husika zinajua.




Wahuni hawa wakiachwa kuendelea kufanya wayafanyayo pasipo mamlaka husika kuchukua hatua ina madhara sana hapo baadaye kuliko wanavyofikiri, tujiulize sababu wanayotumia kufanya wanayofanya, iwe sababu iwayo yote ile je watakapomaliza baa watahamia wapi? Mwalimu aliwai onya kuwa dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, hauachi, iko siku wataanza kuchoma na vituo vya polisi kwa kisingizio hichi ama kingine chochote au maofisi ya Serikali au hospitali kwa si ni kutafuta sababu , na ziko nyingi sana, si kwamba natetea walevi au unywaji pombe, la hasha, bali haiingi alikini vitendo hivyo. 


Wapo wanaodhani ni sababu za imani, mi nadhani sio kweli, si imani kinzani bali ni uhuni, mwanazuoni yeyote aliyesoma vyema vitabu vitakatifu anajua kabisa kwa Mwenyezi Mungu aliumba kila jambo kwa wakati wake, Biblia (kitabu nikisomacho mimi) inasema Mungu aliumba Mbingu na Nchi, Giza na Nuru, Shetani na Malaika, Wema na Wabaya naam bila shaka walevi na wacha Mungu, Peponi na Kuzimu, kila jambo na wakati wake, tujiulize ni kwa nini Mungu aliumba hasi na chanya? je alikuwa anashindwa kuumba hasi peke yake? Mwanzo 1&2




Aliumba yote hayo kabla hata hajamuumba mwanadamu, tujuilize ni kwa nini aliumba hivyo? bila shaka sote kwa imani zetu twaamini kuwa HAKUNA NENO LOLOTE MUNGU HAWEZI FANYA, je wahuni hawa wafanyayo hayo wanajua hii? wamesoma vitabu gani viwapayo kufanya hayo? ni menukuu Biblia lakini naamini ata vitabu vinginevyote, isipokuwa cha shetani (kama kipo) vitakuwa vyakubaliana na usemi huo, na kama Mungu wetu hashindwi jambo je anashindwaje kujitetea katika hili au kutetea waja wake?




Wahenga walisema "Mchelea mwana kulia ulia yeye"

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...