Sehemu ya tamko la serikali lililotolewa na Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja kufuatia hoja binafsi ya Mbunge wa Bumbuli juu ya mgomo wa wauza mafuta uliodumu kwa takriban wiki sasa.
1.
Mheshimiwa
Spika, kufuatia hali iliyojitokeza, EWURA imetoa Compliance Order kwa makampuni manne
ambayo ni BP, Engen, Oilcom na Camel Oil, ambapo wanatakiwa watekeleze hatua
zifuatazo:
(i)
Mara moja wanatakiwa kuanza kutoa huduma
katika maghala yao ikiwa ni pamoja na kuanza kuuza mafuta katika vituo vya
rejareja ikiwemo vituo vilivyo chini ya miliki zao;
(ii)
Waache mara moja kitendo chochote
kitakachosababisha upungufu wa makusudi wa mafuta ya petroli katika soko la
Tanzania; na
(iii)
katika kipindi cha masaa 24 wajieleze kwa
nini wasichukuliwe hatua za kisheria dhidi yao kwa kukiuka matakwa ya Sheria ya
Mafuta pamoja na Sheria ya EWURA.
2.
Mheshimiwa
Spika, baada ya kuisha kwa muda uliotolewa na EWURA, adhabu stahiki
zitatolewa kwa wahusika ikiwa ni pamoja na kusitisha ama kufuta leseni.
3.
Mheshimiwa
Spika, katika hali ya kawaida na kwa mujibu wa Sheria, mtu
asiporidhika na maamuzi ya EWURA anapaswa kukata rufani katika Baraza la
Ushindani (Fair Competition Tribunal).
Hatua hii haijafuatwa hadi sasa na Serikali ingeshauri kwamba masuala kama haya
ni vema yakafuata taratibu za kisheria.
4.
Mheshimiwa Spika; naomba kuwasilisha.
Msaada kwa wadau: COMPLIANCE ORDER yamaanisha nini kwa kimatumbi?
No comments:
Post a Comment