TAASISI ya Tanzania Medicinal Plant Foundation (TMF) kutoka jiji la Mwanza Jimbo la Ilemela imekuja na dawa mpya ya miti shamba inayotibu magonjwa yote ikiwamo Ukimwi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Idara ya Habari Maelezo leo hii asubuhi Mwenyekiti wa TMF Marwa Gonzaga alisema dawa hiyo ya miti shamba inaitwa Tarissa Stinarum inapatika katika jimbo la Ilemela kijiji cha Nyamwilolelwa kata ya Igombe.
Gonzaga alisema walianza utafiti wao mwezi wa Januari mwaka huu baada ya kwenda kwa Babu Loliondo kuona kama kuna tofauti na dawa hiyo ya kwao.
Mwenyekiti alisema kuwa dawa ya Babu Loliondo na ya kwao ni sawa wanatumia miti shamba mmoja uliojulikana huko india miaka ya 1958.
“Babu wa Loliondo anatumia dawa hii tunayotumia sisi na tulikwenda samunge kuangalia tukathibisha na watafiti wa maabara wakathibitisha na sisi tukaendelea na utafiti wetu wa dawa hii ya miti shamba,’ alisema
Alisema dawa hiyo ya miti shamba inatibu magonjwa mengi kama vile Kisukari, Magonjwa ya moyo, Ukimwi na Kansa.
Mwenyekiti alisema dawa hiyo unakunywa mara mbili tu baada ya wiki mbili baada ya kunywa na ni shilling elfu moja kwa kikombe.
kwa hisani wa Mo Blog
No comments:
Post a Comment