Stars mmejifunza nini kwa Mali?
Matokeo ya mechi ya ufunguzi ya fainali ya Kombe la Afrika iliyoanza kutimua vumbi jana kwa wenyeji Angola kuchuana na Mali yaweza kuacha historia fulani kwa kipindi Fulani katika medani ya soka Afrika na dunia kwa muda Fulani.
Si tu kwa mbwembwe za ufunguzi ama serikali ya Togo kuamua kuitoa timu yao baada ya kuvamiwa na majambazi wakielekea mashindano na hatimaye watu watatu kuuwawa au uwezo wa mwenyeji kufunga magori mengi manne na kuongoza kwa kipindi kirefu ata kuwa na uhakika kuwa wameshinda gemu ama uwezo wa timu Mali kurudisha magori yooote manne kwa dakika takribani kumi na moja, si hayo tu.
Bali pengine nadhani ni moyo wa uvumilivu na kutokata tamaa kwa timu ya Mali, kuendelea kupambana na hatimaye kufunga magori mazuri na ya uhakika na kuwaacha wenyeji vinywa wazi, kwa hakika timu ya Mali ni nzuri na wachezaji wake wamejengwa vyema kisaikolojia kiasi cha kutokana tamaa mapema, sikuamini macho yangu kile kilichokuwa kinatokea jana.
Baada ya mechi ile nilijiuliza maswali mengi sana kuhusu timu yetu Taifa Stars, Je wachezaji wetu wangekuwa ndo timu ya Mali wangefanyaje? Pamoja ya kuwa goli ni goli lakini magori mawili ya Angola yalitokana na penati, kwa mtazamo mfupi wa kukata tamaa na kutafuta mchawi Mali wangeweza kusema kuwa mwenyeji kapendelewa na hivyo kuwa na sababu ya kushindwa, je si ndivyo timu yetu ingepata kisingizio na kwa kuwa wote tulikuwa tunaangalia na kuona ni kweli? Hapana shaka kuridhika na kufungwa pia?
Taifa stars inahitaji kujegwa sana kisaikolojia kwenye gemu labda kuliko kitu kingine chochote, kuwa hakuna kukata tamaa ata kama umefungwa goli ngapi na timu gani iwe Brazil au Ivory Coast. Mechi iliyopita na Ivory coast tulikuwa na uwezo wa kuwashangaza kwa kiasi kikubwa lakini nadhani wachezaji wetu pamoja na kusifiwa kufanya vizuri lakini hawakufanya vizuri sana, wengine walikuwa wakionekana kama watazamaji, wakiwaangalia kina Dogba au Cole, laity tungelikuwa na majaribio golini manne kama lile la Tegete tungewaacha vinywa wazi Tembo wa Ivory.
Ushauri wangu kwa kocha ni kuchukua mkanda wa mechi ya jana alinganishe na mechi yetu na Tembo na mechi zooote ambazo tumeshibdwa au hata kushinda pia na kuona ni nini Mali wamefanya ambacho hatuwezi kufanya.
No comments:
Post a Comment