Mama Salma Kikwete awataka wanaume wa mkoa wa Mara kuacha tabia ya kuwapiga wake zao
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanaume wa mkoa wa Mara kuacha tabia ya kuwapiga wake zao bali wawasaidie kufanya mambo ya maendeleo ambayo yatawasaidia kujikwamua kimaisha.
Mama Kikwete aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya siku mbili ya uwekezaji na ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa uwekezaji uliopo mjini Musoma.
“Nilikuwa nasikia kuwa eti wanawake wa mkoa huu wakipigwa na wanaume zao ndiyo wanaonekana kuwa wanapendwa sana sasa sijui kama ni kweli au la, lakini kwa kuwa leo niko na nyinyi wenyeji wa Mara nitajua kama ni kweli ”, alisema.
Tatizo langu mi kwa watani zangu hawa ni hapo, je kinamama si wataona waume zao hawawapendi? nasikia eti ikipita wiki bila kupigwa mama wa kikulya uanzisha zogo mwenyewe na asipopata kichapo basi atarusha jiwe juu ya bati afu atakinga mgongo iliaangukiwe nalo ndo amani inarejea ndani ya nyumba, kweli hayo watani???
No comments:
Post a Comment