Mkuu wa Wilaya ya Morogoro , Said Mwambungu ( mwenye suti) akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Lupanga mara baada ya kumaliza mazungumzo na walimu wa shule hiyo kuhusiana na mgomo wa wanafunzi na kuwataka warejee madarasani wakati uchunguzi wa kina dhidi ya walimu walioongoza kupigiwa kura za maoni ukiendelea kwa ajili ya kuchukua hatua za kinidhamau naa kisheria.
Ikibainika ni kweli waliohusika uenda wakafukuzwa kazi- CWT
Na Theopista Nsanzugwanko
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimesema iwapo itathibitika kuwa walimu watano wa kiume katika Sekondari ya Lupango wamekithiri katika vitendo vya ngono na wanafunzi wa kike wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi.
Aidha,ametaka uchunguzi wa kina ufanyike isiije ikawa ni chuki binafsi za watu wenye nia ya kutaka kuwaaribia sifa walimu.
Akizungumza na Habari Leo, Rais wa Chama cha Walimu Nchini (CWT), Gratian Mkoba alilaani kitendo hicho ambacho kinaendana kinyume na maadili ya ualimu na kusisitiza kuwa yeye hana uhakika na jambo hilo lakini kama ikigundulika wachukuliwe hatua.
“Sisi hatufurahishwi na kitendo hicho kilichoizalilisha kazi ya ualimu,kwani tunaamini kuwa kuwa walimu ambao hawana taaluma ya ualimu bali wameingia tu katika fani hii hivyo wachukuliwe hatua kali ikibainika hata kufukuzwa kazi”alisema Mkoba
No comments:
Post a Comment