TAARIFA KAMILI YA MHE RAIS KIKWETE:
"Nimesikitika sana tumetolewa dakika za majeruhi. Lakini nimefurahi hatua tuliyofikia katika maendeleo ya soka. Sasa tunatambulika na kuheshimika katika ulimwengu wa soka Barani Afrika. Tuongeza bidii. Tusirudi nyuma, bali twende mbele.
Nawapongeza wachezaji kwa bidii na juhudi zao. Nawapongeza walimu kwa kazi nzuri waliyoifanya kuinua kiwango cha soka nchini. Nawapongeza viongozi wa TFF kwa uongozi wao nzuri. Nawapongeza Watanzania kwa kuiunga mkono timu yao. Mmekuwa chachu ya mafanikio haya.
Watanzania wenzangu tusife moyo. Mwanzo mgumu. Tumeanza vizuri na tumefika pazuri. Tuendeleee kuiunga mkono timu yetu. Mimi naahidi kuendelea kuiunga mkono timu yetu mpaka tufika pale tunapopataka sote."
JK
No comments:
Post a Comment