November 11, 2008

SALAMANDER YASIKITISHA WENGI!!

JENGO LA TRA LILILOKARABATIWA NA KUFUNGULIWA HIVI KARIBUNI, WENGI WAHOJI KWANINI SALAMANDER ISINGEFANYWA VIVI?
Wakazi wengi wa jiji wamesikitishwa na kitendo cha kuvunjwa kwa jengo lililokuwa na mgahawa maarufu wa Salamander katikati ya jiji la bongo.
Wengi wamesema kuwa hii ni kupoteza kabisa historia ya jiji hili ambalo kila siku majengo ya zamani ya kihistoria yabavunjwa kwa kasi kubwa kupisha maghorofa marefu mjini humo kwenye msongamano mkubwa wa magari muda wote, lakini pia wanajiuliza kuwa mwekezaji huyu aliahidi kuwa angelilikarabati jengo hilo na kubaki kama lilivyokuwa iwapo tu serikali ingemwambia afanye hivyo, swali je SERIKALI haikupenda au kumtaka afanye vivyo?
angalia nukuu hapo chini toka ktk moja ya magazeti ya kila siku hapa Bongo.
Manji aibana serikali kuhusu Salamander na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Quality Group Limited (QGL), imesema mkanganyiko wa wizara mbili, kuhusu ununuzi wa jengo la Salamander, Dar es Salaam, unaweza kumalizwa ndani ya serikali yenyewe. Mkurugenzi Mtendaji wa QGL, Yusuf Manji, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema anaheshimu historia ya Tanzania, na kamwe kampuni yake haitaharibu jengo linalohusiana na historia ya taifa. Ni kwa sababu hiyo, alisema tangu Agosti 26, 2006 kampuni ilipozuiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kuvunja jengo hilo katika notisi ambayo haikuwa na nguvu kisheria, bado kampuni iliheshimu uamuzi huo. Alisema QGL inatoa nafasi kwa vyombo husika kufanya utafiti na kuondoa wasiwasi kwa walengwa.
“Pia QGL inatoa nafasi kwa serikali kufanya tathmini ya uamuzi wake ya kwamba jengo lijengwe upya, au likarabatiwe na kuachwa kama sehemu ya makumbusho ya kihistoria. “Na kama uamuzi utaridhia jengo la Salamander libomolewe, QGL inakusudia kujenga jengo jipya la ghorofa 22 katika eneo hilo. “Kwa upande wa pili, kama uamuzi wa serikali ni kuliacha jengo hilo kama lilivyo, QGL inaheshimu uamuzi huo wa serikali na kuomba kurejeshewa malipo iliyofanya pamoja na gharama nyingine,” alisema Manji.
Pia alisema ni vema jamii ikafahamu kuwa Msanifu wa Serikali alifanya utafiti wa jengo hilo na kubaini kuwa ni chakavu na hatari kwa maisha ya binadamu.

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...