December 7, 2008

Yaliyojili mahafali ya 38 UDSM

Dada Janeth Tesha alikuwa Mhitimu pekee wa Dgrii ya Uzamili ya Sayansi ktk Uhandisi Nishati Umeme au Masters of Science in Electrical Power Engineering. Hawa ni Digrii ya Biashara (Bachelor of Commerce) walikuwa 543. wakti fani kama hizo za uhandisi na hasa za umeme zilikuwa na mtu ama mmoja au saaaana watatu, ktk fani nyingine kama hii ya Biashara wahitimu walikuwa lukuki.
TUJADILI WADAU:

Je kwa mtazamo na mwenendo huo hapo juu wamaanisha nini kwa mustakbali wa taifa letu ktk karne hii ya sayansi na teke linalotujia?

for Science and Technology era we are in, what does this mean?

2 comments:

Markus Mpangala said...

duu mkuu hakika hiyo inaonekana wametulia na wafurahia, LAKINI hapo kuna hofu kwamba namna gani watapata kazi au kufanya kazi. katika nchi yetu kila mhitimu anabeba furha na JOHARI YA MATUMAINI{AUDACITY OF HOPE, kama alivyosema Barack Obama kitabuni mwake.} lakini nchi yetu bado ina kasoro kadhaa ambazo tunaamini zitaondoka iwapo tuweka dhamira ya kuyaondoa. Matumaini waliyonayo dada zangu na kaka zangu walionitangulia hawa{maana sisi tunasota shauri ya mgomo, tungojee kwanza} wanaonekana wana kila sababu ya kupata kazi nzuri na maslahi mazuri ILA kuna tatizo mahala kwamba wengi wengi tunavyeti vikali na mahiri lakini utendaji ni duni, hili linachangiwa na mazingira ambayo msomi mwenyewe anasoma kwani muundo wa elimu yetu imejngwa katika kukariri hoja za wabunifu au wanafalsafa bila kuitumia katika uhalisia wa mambo. tunamezeshwa mengi na kuyatapika kwa mikogo kama siyo kumung'unya halafu kumbe bado tuna kasoro kadhaa. OMBI langu SOMENI MAONI YA JENERALI ULIMWENGU mtabaini hiki ninachokisema, hasa katika mfululizo wa makala zake zilizopita. CHUO KIKUU sawa lakini binafsi nipo mwaka wa pili POLITICAL SCIENCE ANA PUBLIC ADMINISTRATION bado natilia shaka mfumo wetu wa elimu ni mbovu kupindukia. tutashindana kwajua wanafalsafa na wataalamu wengine lakini je tupo katika uhalisia wa mambo?
JAMANI MADA MUHIMU SANA KWA MUSTAKABALI WA NCHI YETU

Anonymous said...

Haishangazi mkuu kuona kila siku tuna shida ya umeme katika nchi iliyojaariwa mito, maziwa na bahari ya kumwaga lakini jua liwakapo mwezi mmoja ni mgao wa umeme nchi nzima.

pia jinchi hili la bongo limeaariwa sana hata twaweza zalisha umeme kwa upepo au windmills lakini sote tumengangana na biashara na siasa tu, ukingalia takwimu za wanaohitimu ktk vyuo vyetu mwelekeo ndo huo tuna kazi sana kupiga hatua ktk karne hii tuiishimo.

asante mzee Bongo pix kwa kutupa data hizi wito kwa wadau tuchangie ktk hili ili kuleta mustakbali mwema wa taifa letu.

MDAU CHINA.

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...