October 20, 2008

TUDURUSU kiduchu yalojili TARIME

Vumbi la Uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime limetuwama kwa sasa na mshindi na mshindwa ameshajulikana, si vibaya kudurusu kwa chati yaliyojili huko na mstakbali wa Jimbo au Nchi yetu kwa upande mmoja na siasa za vyama kwa upande mwingine.
Kwa hakika yaliyojili huko ktk kipindi chote cha kampeni hata siku ya uchaguzi yenyewe, gharama na maelkopta yaliyotumika kwa jimbo hilo tu si madogo hata kidogo kiasi cha kuyaacha yapite tu.
Huu nadhani waweza kuwa uchaguzi mdogo uliowahi kutumia gharama kubwa kuliko mwingine wowote ktk historia ya taifa letu changa (nasema nadhani kama sivyo naomba kukumbushwa) na masikini ambalo wapo wenzetu wanaopata japo mlo mmoja tu kwa siku na kwa taabu sana tena ndani ya Tarime yenyewe lakini kwa kipindi kifupi tu wameshuhudia matumizi ya kukidhili ya fedha mbele ya macho yao huku wakiambulia vumbi tu.
Mbali na gharama jambo lingine ni siasa za chuki zilizo kidhiri jimboni humo, kwa hakika hili lilikuwa ni tatizo kubwa sana si tu kwa wanatarime wenyewe bali hata sie tulioenda kuripoti habari hizi hatukuwa na amani kabisa, kwa macho yetu tulishuhudia unyama wa kutisha ukitendeka, mtu kukatwa mapanga mbele ya adhala pasi na kujali lolote kwa mkataji, tumeshuhudia damu ikimwagika mbele ya macho yetu, pengie kwa wanatarime wanaweza wasishangazwe sana na hilo kulingana na historia yao na hasa yale ambayo yamekuwa yakijili hapo, lakini kwetu sie hilo lilikuwa la kuogofya sana.
Hali hii ilituwakati mgumu sana kutekeleza majukumu yetu na kwa kweli ilitutia woga mno, pengine ndo maana baadhi yetu wengine waliamua kuegemea moja mbali na mwingine pengine ni ktk kutafuta ulinzi lakini kwetu sie tuliokuwa kati kwa kati hali ilikuwa ngumu sana na hata utendaji wetu uliadhiriwa kwa kiwango kikubwa sana.
Hizi zilikuwa ni siasa za chuki ambazo sikupata kuzishuudia wakati mwingine wowote hapa Bongo, za kushindwa kuvumilia kusikia mtu akitoa kile ambacho pengine kwa mtazamo wako ni utumbo au upuuzi na kuamua ama kumpiga mawe (kama yalomkuta Mch Mtikila na Mbowe) au kumchalnga kwa mapanga kama wale majeruhi wanne au hata kumzuia Mh Waziri kuona majeruhi tu.
Kwa hakika hizi si aina ya saisa ambazo tungependa tuwe nazo Watanzania na zaidi ya yote tufanye kila tuwezalo siasa hizi zisijirejee tena jimboni humo au penginepo popote nchini mwetu kwa hazitufai na si utamaduni wetu hata kidogo.
MUNGU BARIKI TANZANIA

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...