August 8, 2008

JIMY ELIAS AFARIKI

Mwandishi wa siku nyingi Jimmy Elias afariki MWANDISHI wa habari wa siku nyingi, Bw. Jimmy Elias (41) amefariki dunia juzi asubuhi katika Hospitali ya Amana, Dar es Salaam, baada kuugua kwa takribani mwezi mmoja. Mmoja wa ndugu wa marehemu, Bw. Richard Mwaikenda, alisema Jimmy (pichani) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya matumbo na alikuwa akiendelea na matibabu nyumbani lakini alipozidiwa alipelekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu zaidi. Mwili wa marehemu unatarajia kuagwa KESHO mchana saa sita nyumbani kwake Kiwalani Bombom na baadaye kusafirishwa kuelekea katika kijiji alipozaliwa Ngana, wilayani Rungwe mkoani Mbeya tayari kwa mazishi yatakayofanyika Jumapili. Hadi mauti yanamkuta alikuwa Meneja Mauzo wa gazeti la Ngurumo za Simba na jarida la StarSport tangu yalipoanzishwa.pia katika kipindi cha uhai wake aliwahi kuandikia magazeti ya Dar Leo (zamani Majira Jioni) na Mfanyakazi. Ameacha mke Bi. Mary Katendele na watoto watatu ambao ni Boniface, Jackson na Staford.Katika uhai wake alikuwa mpezi mkubwa wa mpira wa miguu ambapo alikuwa ni mwanachama hai wa Klabu ya Simba. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
Posted by Picasa

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...