April 28, 2008

KIJANA ADAI ANA VICHWA 50 ZAIDI!!!!

Aliyekutwa akitafuna kichwa cha mtoto atoa madai mazito.
Kijana Ramadhani Seleman Mussa (18), anayedaiwa kukutwa akitafuna kichwa cha mtoto Salome Yohana (3), amedai kumiliki vichwa vingine 50. Mbali ya kumiliki vichwa hivyo, pia kijana huyo amedai kwamba, amekuwa `akitengeneza` ajali barabarani kwa njia za kishirikina kwa lengo la kujipatia damu ya kunywa.
Alitoa madai hayo jana katika kituo kidogo cha polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar es Salaam ambako anashikiliwa pamoja na mama yake mzazi, Khadija Ally na baba yake wa kufikia, Lucas Kibaya.
Akiwa kituoni hapo, kijana huyo alionekana akitoa maelezo hayo kwa ujasiri na pasipo wasiwasi wowote. Hata hivyo, kutokana na maneno mazito na yakutisha aliyokuwa akiyatoa, polisi walilazimika kuwaondoa baadhi ya watu katika chumba cha mahojiano. Watu walioshuhudia mahojiano hayo , waliiambia Nipashe kuwa, Ramadhani aliwaeleza polisi kwamba, anamiliki vichwa hivyo 50 kwenye maeneo tofauti hapa jijini Dar es Salaam na mkoani Mtwara alikodai alikuwa akiishi na baba yake mzazi.
Aidha, alidai kuwa ametega`kombora` la kichawi la kusababisha ajali katika barabara ya Morogoro pembezoni mwa daraja la Manzese ambalo hutumiwa na watembea kwa miguu. Madai hayo yaliungwa mkono na majirani wa sehemu aliyokuwa akiishi kijana huyo, eneo la Segerea kwa Bibi. Mmoja wa majirani hao, Bw. Sadi Marando, alidai kuwa, kijana huyo alimweleza kwamba, kila baada ya miezi mitatu, hupata kiu ya kunywa damu ya mtu.
Bw. Marando, amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kumshikilia mama wa kijana huyo kwa madai kwamba, Ramadhani alikuwa akisema siku zote kwamba, kazi zote za ushirikina hushirikiana na mama yake Khadija Ally. ``Kijana yule ni hatari ukisikiliza masimulizi yake unaweza kukimbia, hapa mtaani alikuwa na maisha ambayo kwa kweli yalikuwa ya kutisha, si mtu wa kawaida,`` alidai Bw. Marando.
Bw. Marando, alisema kutokana na kijana huyo kutoonekana kama binadamu wa kawaida, majirani walikuwa wakimhoji kila mara na kuna siku alisema kwamba wanacho kikundi chao chenye watu 10 akiwemo mama yake na kwamba yeye ndiye kiongozi.
Alisema katika mfululizo wa vituko vya kijana huyo, Alhamis iliyopita alitaka kumchinja mdogo wake, Pascal Lucas. ``Alikuwa ameshamkanyaga chini kama kuku na kuanza kumchinja, bahati nzuri majirani wakafanikiwa kumkamata, nadhani kiu ya damu iliendelea ndiyo maana alimteka na baadaye kumuua Salome,`` alisema Bw. Marando.
Ramadhani amenukuliwa akisema kwamba `makao makuu` ya kundi hilo yako mkoani Mtwara na wameweka `matawi` maeneo ya Manzese Darajani na Buguruni, jijini Dar es Salaam. Polisi mmoja wa kituo cha Stakishari aliyeomba jina lake lisitajwe, alisema Ramadhani bila woga amesisitiza kwamba, si mara yake ya kwanza kula nyama ya mtu na kwamba ataendelea kwa vile nyama za watu ndizo humpa nguvu katika mambo ya kishirikina.
Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Bw. Charles Mkumbo, alisema upelelezi na maneno yaliyozungumzwa na kijana huyo ni siri yao kwa ajili ya kutengeneza kesi. Alisema hata kama kijana huyo anadaiwa kutoa maneno hayo, polisi hawatishiki na watamfungulia kesi kama muuaji wa kawaida. ``Tunachopeleleza sasa ni siri yetu, tunatafuta ushahidi na kujua mazingira ya tukio hilo na sisi tutamshughulikia kama muuaji mwingine yeyote na kamwe suala la uchawi kwetu halipo,`` alisema Kamanda Mkumbo. Alipoulizwa kwamba kama polisi hawasadiki taarifa za uchawi ni kwanini wanawashikilia wazazi wa kijana huyo, Kamanda Mkumbo alijibu kwamba, wanawashikilia kwa kutambua kuwa, huenda wanajua mengi juu ya mtoto wao kutokana na kuishi naye kwa muda wote. Kuhusu mazishi ya marehemu mtoto Salome, Kamanda huyo alisema polisi haina neno juu ya hilo bali inasubiri taratibu za maziko zitangazwe na familia. Hata hivyo, alisisitiza kwamba, kabla ya maziko, lazima mwili wa marehemu ufanyiwe uchunguzi ambapo polisi wameomba ndugu wapeleke mwakilishi atakeyeshuhudia. ``Ndugu wakiwa tayari, muda wowote waje tuwakabidhi mwili, lakini kwaza tutaufanyia auchunguzi,`` alisisitiza Kamanda. Nipashe ilitembelea familia ya marehemu huyo huku mama na baba wa mtoto aliyeuawa kwa kuchinjwa, wakiwa wamegubikwa kwa majonzi. Mama wa mtoto huyo, Bi. Pendo Dunstan, alisema majonzi aliyo nayo hawezi kuyaelezea. ``Ni Mungu tu anayejua moyo wangu unaugua kwa jinsi gani,`` alisema kwa masitiko makubwa. Naye baba wa marehemu, Bw. Yohane Majana, aliwataka polisi wamuachie huru kijana huyo anayedai kuwa ni mchawi ili na yeye amwonyeshe uchawi wa kisayansi. ``Wamwachie! Mimi naomba aachiwe huru ili nikutane naye ana kwa ana tuone,`` alisema.
Kuhusu mazishi, Bw. Majana alisema bado wanajikusanya ili kupata fedha hasa ikizingatiwa kwamba familia yao ni maskini. Alisema ndugu na jamaa walitarajiwa kukutana jana kwa ajili ya michango na kwamba wanatarajia mazishi yafanyike leo eneo la Segerea. Wakati huo huo, Godfrey Monyo na Karama Kenyunko wanaripoti kuwa, polisi jijini Dar es Salaam, inawashikilia wazazi wa mtoto aliyekutwa na kichwa cha mtoto katika mfuko wa rambo. Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Bw. Charles Mkumbo, alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo na kwa kuanzia wameanza kwa kuwashikilia wazazi wa mtoto huyo. ``Tumewashikilia wazazi wa mtoto aliyesababisha mauaji hayo na mtoto mwenyewe pia tunaye kwa hiyo tunaangalia nini kifanyike ili kubaini chanzo cha tatizo hilo,`` alisema. Kamanda Mkumbo alisemapolisi hawaamini kama suala hilo ni la uchawi bali ni tukio la uhalifu kama mengine na kuwataka wananchi kuwapa muda ili kulifanyia uchunguzi kwa kina.
Alisema uchunguzi utakapokamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara moja kujibu tuhuma hizo.
Jumamosi ya wiki iliyopita, kijana Mussa (18) anayedaiwa kuingia jijini Dar es Salaam akitokea Mtwara, alinaswa akiwa na kichwa cha mtoto. Mtoto huyo wa kike, Salome Yohana, alipotea nyumbani kwao Tabata Segerea, wiki iliyopita na baadaye kiwiliwili chake kilikutwa katika choo cha nyumba ya jirani kabla ya kupata taarifa za kuonekana kwa kichwa chake hospitali ya Taifa Muhimbili. source Nipashe

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...