November 3, 2007

"Twende Mzee Mwenzangu tukawashuhudie vijana wanavyotoana kamasi" Wastaafu Mkapa na Mwinyi picha hii imenikumbusha kamakala kapya ka Ncheme, nchicheme ktk gazeti jipya la raiamwema hebu kasomeni kwa wale ambao hamjapata fursa ya kukasoma. LETE vitu Mzee General World. mmmmhhhh haya Masikini Mzee Ali Hassan Mwinyi! Ncheme, nchicheme? Oktoba 31, 2007 TUNGEKUWA tumejaaliwa uungwana na Mwenyezi Mungu, nasi tukawa ni watu wa kukiri makosa yetu na kisha tukawa na moyo wa kutaka radhi wale tuliowakosea, basi Watanzania wengi tungekuwa tumekwisha kuunga ujumbe wa watu wasiopungua 500 kwenda kuanguka chini ya miguu ya Mzee Ali Hassan Mwinyi huku tukimwomba atusamehe kwa makosa makubwa tuliyomtendea. Ujumbe huo ungepaswa uongozwe na wahariri na wasanifu wakuu wa tahariri katika magazeti ya miaka ya mwanzo ya 1990, kwa sababu sisi ndio hasa tulikuwa msitari wa mbele katika kutenda makosa hayo dhidi ya mzee huyo ambaye tulimbatiza jina la “Mzee Ruksa”. Kosa kubwa tulilotenda dhidi ya Rais huyo wa Awamu ya Pili ilikuwa ni kumhusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi, hata kuwafanya wasomaji wa magazeti yaliyochapishwa wakati huo, waamini kwamba kilichokuwa kikifanyika Ikulu ulikuwa ni uharamia wa hali ya juu. Sasa tunajua kwamba yote haya hayakuwa kweli. Haiwezekani kusema kwamba Mzee Mwinyi hakuwa na dosari, kwani kusema hivyo ni kumwondoa kwenye kundi la binadamu. Alikuwa na dosari zake na udhaifu wake, na hayo bado anayo hadi leo, kwa ilivyokuwa wakati akiwa Ikulu. Lakini pia ni kweli kwamba sehemu ya udhaifu wake ilitokana na wema na upole wake katika mazingira ya “manyang’au” aliowaamini na ambao hawakusita kuutumia upole wake na jina lake kufanya walivyotaka kwa kumsingizia yeye. Leo hii sote tunajua kwamba tulimwonea sana Mzee Mwinyi kwa kumbebesha mambo yasiyokuwa yake. Na wala si yeye peke yake aliyekumbwa na uonevu huo bali pia mkewe, Bi Sitti Mwinyi, ambaye naye alihusishwa na kila aina ya maovu kutokana na uvumi ulioenezwa na baadhi ya vyombo vya habari. Baadhi tutakumbuka pia kwamba Mzee Mwinyi aliwahi kulalamika hadharani kwamba uvumi ulikuwa umeenezwa kuhusu yeye kumwoa kigori mdogo kwa kumfanya aache shule… kila aina ya uvumu na uzushi. Mzee huyu muungwana alivumilia, akavuta subira, akasamehe. Haishangazi kwamba amebaki kuwa kipenzi cha Watanzania kutokana na upole, unyenyekevu na uadilifu wake. Tunajua sasa kwamba, ingawaje vitendo vya ufisadi vilitendeka chini ya uongozi wake, yeye mwenyewe binafsi hakuhusika moja kwa moja. Baada ya Mzee Mwinyi kuondoka madarakani ndipo nchi hii imepata bahati mbaya si tu ya kuendelea kuelemewa na vitendo vya ufisadi katika safu za uongozi, bali pia mkosi wa kuwa na ‘kiongozi’ mkuu anayesimamia ufisadi huo kwa kushiriki yeye mwenyewe binafsi kuunda kampuni ya biashara na kuisajili rasmi kwa anwani ya ofisi ya umma, na hata kujihaulishia umiliki wa kampuni ya serikali na kuiandikisha kwa jina lake na familia yake na maswahiba zake. Tumshukuru Mungu tunayo Katiba inayoweka mipaka ya mihula ya uongozi, la sivyo baada ya mihula mitano tungeikuta nchi imehamia bara jingine kwa jinsi tamaa za wakuu zilivyozidi na jinsi matumbo yao yalivyo na nafasi za kujaza. Kisha tumshukuru Mzee Mwinyi kwa uungwana wake, na mwisho tumwombe radhi kwa jinsi tulivyomdhalilisha.

1 comment:

Anonymous said...

agwe... ebwna naita john kutoka kinshansa. nimepata jina la blog yako kupitia patric du mzee endela
kutupa nondo kali namna hii. tunafrijik sanaa.

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...