January 10, 2010

Siku nyingine kadhaa za mashaka Jo'burg

Dar au Bongo kwa ujumla kuna uhalifu, lakini bado mtu aweza tembea kwa kujiamini mchana popote na jioni kwa baadhi sehemu akiwa na vitu vyake muhimu kama simu au kamera, kwa sisi wanahabari wakti mwingine twapanda daladala na vifaa vyetu na hata kuingia sehemu kama Manzese, Mwananyamal, Tandika na kwingineko pasi kuwa na mashaka saana hasa wakti wa mchana, lakini katika Jiji hili la Taifa kubwa la Afrika yaani Jo'burg hali si hivyo.
Jana tulijaribu kutoka na kuninginiza vifaa vyetu katika moja ya joint muhimu na maarufu sana ijulikanayo kama The Mall of Rosebank, hii ni kama vile pale Mlimani city hapo bongo japo ni kubwa mara kadhaa kulinganisha na MC, wakti tunaingia tu mara akatokea bwana mmoja mzungu na kutuuliza nyie ni wageni hapa?
Mwenyeji wetu akamjibu ndio na hapana, yule bwana akasema " jihadharini mnavyotembea na kamera zenu hizo" nikashangaa sana, yaani hata sehemu kama hii bado waweza kuporwa?
Hii ndo hali halisi ya maisha hapa Jo'burg, kuporwa simu, kamera na kukabwa pengine ata kuuwawa ni kitu cha kawaida kabisa, na yote yaweza kukutokea mbele ya umati na hakuna msaada.
Jambo moja nimegundua kulingana na maelezo ya dereva taxi Bw Titi alokuja nichukua eapoti ni kuwa vijana wengi hasa weusi wamekata tamaa na maisha, kwani wanaona kuwa hawana nafasi katika keki ya Taifa na kuwa wanaonufaika ni weupe na wanaotoka bara asia, wanadhani kuwa serikali haiwajali.
Titi anasema weupe kutokana na uwezo wao ama kuinuana kwa makusudi wenyewe kwa wenyewe wamekuwa wakinunua maeneo na biashara muhimu katikati ya majiji kama Jo'burg hivyo weusi kukosa fulsa kama hizo.
Hili yawezekana kabisa ni time bomb langoja kuwashwa tu lilipuke?
Bongo twafanyaje kuhusu hali kama hii? twajiadhari vipi nayo? maana sidhani kuwa hii ni ya hapa Bondeni tu. nasema tena sidhani!

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...