Hii sasa ni hatari sana wadau, hivi ni tamaa gani hii ya pesa hata hatuhurumiani? tumekuwa tukiwalaumu wachina kwa kila bidhaa feki lakini hebu tujiulize je sio sisi wabongo na hasa ndugu zetu wafanyabiashara ambao ndo wananunua bidhaa hizo ama pengine wanawashawishi wao wachina kutengeza mabidhaa feki na hatimaye kuziingiza sokoni?
Hii ni tamaa gani ya pesa hata ufikilii ndugu zako? je bidhaa hizo feki si ni ndugu zako ndo wanatumia? na je si ni hao pia ndo wanadhurika?
Hii inasikitisha saaana.
· Polisi wakamata za Shilingi milioni 60
· Za Arusha zaletwa Dar kwa hatua zaidi
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekamata malori manne yakiwa yemesheheni taulo za usafi za wanawake feki (Always) zenye thamani ya Sh. milioni 60 zinazodaiwa kuingizwa kinyume cha sheria.
Malori hayo aina ya Fuso moja na Canter tatu, yalikamatwa juzi eneo la Jangwani, jijini Dar es Salaam yakiwa na shehena za bidhaa hizo ambazo zilikuwa katika makasha madogo 2,750
No comments:
Post a Comment