Kauli ya Makame yaichanganya ZEC
MKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Salum Kassim amesema haamini kama mwenyekiti wa taifa, Jaji Lewis Makame anaweza kujitoa katika suala la Zanzibar na kutaka jamii iilaumu Zec kwa vurugu zinazoendelea kisiwani Pemba.
Juzi Jaji Makame alisema mjini Dodoma kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) haistahili kuhusishwa na vurugu zinazoendelea kisiwani Pemba, ambako wananchi wanagomea zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura wakipinga matumizi ya kitambulisho cha Uzanzibari Ukaazi kama kigezo kikuu.
"Kama Nec ingekuwa msimamizi wa uandikishaji kwa ajili ya chaguzi hizo (za Zanzibar), ingestahili kubeba lawama, lakini Zanzibar kuna tume huru... Zec ambayo inasimamia taratibu zote katika daftari hilo, ndiyo inapaswa kulaumiwa,"alisema Jaji Makame juzi.
source: mwananchi
No comments:
Post a Comment