September 16, 2009

Bibi miaka 107 atafuta CHUO cha 24

Wook Kundor akiwa na mumewe wa sasa, Muhammad Noor Che Musa
Bibi mwenye umri wa miaka 107 wa nchini Malaysia ambaye alishaolewa na kuachika mara 21 amesema yuko tayari kuolewa na mwanaume mwingine kwa mara ya 23.
Ajuza huyo anahofu kwamba huenda mume wake wa 22 anaweza kumkimbia na kutafuta mwanamke mwingine mwenye umri mdogo.
Baada ya kuolewa na wanaume 21 na kuachika, bibi mwenye umri wa miaka 107 wa nchini Malaysia amesema kuwa anahofia kukimbiwa na mume wake wa 22 anayeishi naye hivi sasa ambaye miezi miwili iliyopita alikamatwa akitumia madawa ya kulevya.
Bibi Wook Kundor alipata umaarufu duniani baada ya kuolewa kwa mara ya 22 na mwanaume ambaye amemzidi jumla ya miaka 70.
Hivi sasa bibi Wook hana imani kabisa na mumewe Muhammad Noor Che Musa mwenye umri wa miaka 37 ambaye hivi sasa yuko kwenye kituo cha kurekebisha tabia akipatiwa matibabu ya kuacha utumiaji wa madawa ya kulevya.
Bibi Wook ameishaanza kusaka mume wa 23 kwa sababu anahofia Muhammad akishatoka kwenye kituo hicho na kuacha tabia yake ya kutumia dawa za kulevya anaweza kumkimbia na kutafuta mwanamke mwingine wa rika lake.
"Katika siku za hivi karibuni kuna hofu imeniingia" alisema bibi Wook huku akiwa ameshikilia picha yake.
"Najua kwamba mimi ni mwanamke niliyezeeka. Sina umbile la kuvutia tena na kwa umri wangu siwezi kumvutia mwanaume yoyote"
"Nia yangu ya kuolewa tena ni kuepuka upweke na si kwa sababu yoyote ile" alisema Wook na kuongeza kuwa anajihisi mpweke sana wakati huu ambao mumewe yuko mbali.
Bibi Wook alisema kuwa angependa kusherehekea sikukuu ya Eid el-Fitr wiki ijayo akiwa pamoja na mumewe.
Wook alisema kuwa ana mpango wa kumtembelea Muhammad kwenye kituo chake cha kurekebisha tabia jijini Kuala Lampur iwapo majirani zake watampeleka huko kwa gari.
Muhhamad alifunga ndoa na bibi Wook miaka mitatu iliyopita akisema kuwa urafiki wa karibu na heshima uligeuka kuwa mapenzi ya kweli.

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...