June 12, 2007

Tuliyojifunza katika asazi zote ni mengi mno ila kwa leo nitazungumzia jinsi idara hii inavyofanya kazi na wapiga picha na watu wa usalama ambalo limekuwa ni tatizo sana kwetu bongo. Huyu ni Julia Fassbender wadhifa wake ni Visual Advisor, kwa fani ni mpiga picha na amewai kuwa mpiga picha mkuu wa serikali, kwa wadhifa wa sasa yeye ndiye anayehusika na kuakikisha upatikanaji wa picha za viongozi wa serikali na kuandaa mazingira ya picha wapi ipigwe na kuakikisha kunakuwa na mwanga na mazingira bora. kwa kufanya ivyo na kwa kushirikiana na watu wa protokali anahakikisha hakuna muingiliano wowote wa watu wa usalama pamoja na kupanga eneo mwafaka kwa wapigapicha si wa serikali bali wote wanaokuwepo kuweza kupata picha nzuri. Mkutana wa G8 ulioisha karibuni ulikuwa na wapiga picha zaidi ya 2,000 toka kote ulimwenguni lakini kila mmoja alipaga picha pasi na muingiliano na watu wa usalama, waweza dhania hawakuwepo vile, lakini sote twajua kuwa pengine walikuwa mara nane ya wapiga picha, swali je wako wapi? Kwa wapigapicha na watu wa protokali au usalama liko jambo la kujifunza hapa, kwa maneno yake anasema picha nzuri si suala la bahati bali lapangwa kabla. pia lakufurahisha ni kwamba wanaprotokali ndio wanaotaka viongozi wao wapate picha nzuri kadiri iwezekanavyo hivyo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wapiga picha, wakisha kukagua vya kutosha (kama wafanyavyo bongo) na kukurusu kuwa eneo la tukio na wawekapo eneo la wapiga picha hakuna yeyeto anayeruhusiwa kukatiza kati ya wapigapicha na viongozi ivyo kuweza kupata picha nzuri. kumbuka mpigapicha ni muweka kumbukumbu za baadaye, picha nzuri tuzionazo leo ziliandaliwa mazingira mazuri ya mpigapicha kuzipata.

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...