October 17, 2011

Tuukemee kwa nguvu zote ukatili huu




VITENDO vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) vimeibuka tena wilayani Geita mkoani Mwanza, baada ya mlemavu mmoja wa ngozi kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kulia pamoja na kukatwa mkono wa kushoto.

 
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang’hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.

 
Akisimulia mkasa huo, mlemavu huyo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita akiuguza majeraha yake, alisema alikumbwa na mkasa huo saa 1:40 usiku akiwa nyumbani kwao ambapo alivamiwa na mtu mmoja waliyekuwa wanakula naye chakula nje ya nyumba.

 
Akizungumza kwa shida katika kitanda namba 5 alikolazwa, alisema siku ya tukio saa 12 alifika nyumbani kwao mtu huyo akidai amekwenda kuangalia ng’ombe wake waliokuwa wamepotea ambapo walianza maongezi na yeye juu ya upotevu wa ng’ombe hao.

 
‘‘Wakati tuko nje na baba, mtu huyo alifika na kubisha hodi kisha tukamkaribisha tukampa kiti akakaa ndipo akaanza kutueleza kuwa anawatafuta ng’ombe wake waliopotea machungani.
 

Tukaendelea kuzungumza naye hadi tulipoletewa chakula hapo nje tukaanza kula,’’ alisema na kuongeza: ‘‘Ghafla mvua ikaanza kunyesha ikabidi tuhamie ndani, baba akawa amechukua ugali akatangulia ndani mimi nikabeba mboga yule mtu akabeba kiti chake, wakati tunaingia ndani nilikuwa katikati ya baba na mtu huyo, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida kabla sijaingia ndani yule mtu akanishika na kunivuta nje”.

 
Alisema baada ya kuvutwa mtu huyo alianza kumkata mkono wake wa kushoto upande wa begani wakati huo akiwa amelala chini akijitupatupa na baada ya kuona ameshindwa kuukata na kuunyofoa mkono kuanzia kwenye kiganja, akaacha na kuanza kuukatia tena kwenye kiwiko.

 
“Aliposhindwa pia kuukatia kwenye kiwiko aliamua kuugeukia mkono wangu wa kulia na kukata vidole vyangu vitatu vya mkono huo na kuvinyofoa kabisa, wakati huo baba alishindwa afanye nini akabaki kukimbilia huku na kule na wakati huo kaka yangu alikuwa amejificha kwenye nyumba nyingine na kilichonishangaza sana ni kwamba pamoja na kupiga sana kelele za kuomba msaada hakuna mtu hata mmoja aliyejitokeza kwa ajili ya kuja kunisaidia,” aliongeza kusema.

 
Akizungumzia tukio hilo baba mzazi wa mlemavu huyo, Robert Tangawizi (36) alisema wakati tukio hilo linatendeka alikuwa kama vile amechanganyikiwa na kushindwa kabisa kumuokoa mwanawe muda wote wa purukushani kati yake na mhalifu huyo na kwamba alishikwa na bumbuwazi na hasa baada ya kumuona mtu ambaye walikuwa wanakula naye chakula kwenye meza moja amegeuka mhalifu kwa mwanawe.

 
“Yaani kweli mimi sijui hata kwa kweli nashindwa hata kuelezea tukio hili, kwa sababu nashangaa kwamba mtu ambaye tumemkaribisha vizuri na kumpatia kiti kwa heshima zote natukaanza kula naye chakula ghafla anageuka na kuwa muuaji na kufanya kitendo cha kikatili kama hiki nilishindwa kabisa nifanye nini, kwa sababu kwa muda wote sikuamini kama kweli ni mtu huyu huyu ndiye alikuwa akifanya jambo hili,’’ alisema baba mzazi wa mlemavu huyo.





Source: Habari Leo







No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...