TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA WATANZANIA-GAUTENG
Mkutano Mkuu wa watanzania waishio Gauteng ulifanyika tarehe 14 Machi 2010
kwenye ukumbi wa Kempton Park Civic Centre, Kempton Park, Johannesburg,
Afrika Kusini na kuhudhuriwa na watanzania wengi pamoja na Kaimu Balozi wa
Tanzania nchini Afrika Kusini, Peter Kabissa.
Pamoja na mabo mengi yaliyojadiliwa, mkutano huu ulipitisha katiba ya
jumuiya na kuchagua viongozi wa kudumu wa jumuiya hii.
Wafuatao
waliochaguliwa kuwa viongozi wa umoja huu:
1. Dk. Faustine Ndugulile-Mwenyekiti
2. Bw. Laurean Rugambwa-Makamu Mwenyekiti
3. Bi. Josephine Mshilla-Katibu Mkuu
4. Bw. Khalfan Kipemba-Katibu Mkuu msaidizi
5. Bw. Joseph Mshilla-Mweka Hazina
6. Bw. Kassim Kissagalah-Mweka Hazina msaidizi
7. Bw. David Mataluma-Katibu wa utamaduni na burudani
Wajumbe kamati ya utendaji
8. Dk. Robert Ngude-Mwakilishi wa kundi la wafanyakazi
9. Bw.Vincent Malugu-Mwakilishi wa kundi la vijana
10. Bw. Abuu Chenja -Mwakilishi wa wafanyabiashara
11. Bi. Jane Gitonga-Mwakilishi la kundi la kinamama
12. Bw. John Sagati-Mwakilishi wa kundi la wanafunzi
13. Bw. Jumanne Fikha-Mwakilishi wa Ubalozi
Viongozi waliochaguliwa wanatarajia kukutana hivi karibuni na kuweka
mikakati ya kuiimarisha jumuiya hii.
IMETOLEWA NA UONGOZI
TAREHE 16 MACHI 2010
1 comment:
sijaelewa madhumuni ua umoja huo ni nini kwa sababu nilifika huko mara kadhaa na nimekuta wabongo wengi hasa vijana waliotoroka makwao wana matatizo makubwa, hawataki kusoma, wauza unga na ni wezi na majambazi. Ingawa sio wote, lakini wengi wao wamepoteza dira na kujiingiza kwenye makundi hayo.
Post a Comment