Siku tu moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusema kuwa Kampuni ya Development Entrepreneurdhip For Community Initiative(DECI) ni upatu na inaendeshwa kinyume cha sheria za nchi uongozi wa juu wa kampuni hiyo umeomba kukutana na viongozi wa juu wa taifa na Benki Kuu ya Tanzania(BOT).
Meneja wa Masuala ya Ufundi na Ushauri wa Kitaalamu wa DECI, Arbogast Kipili akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari ( MAELEZO)alisema hawako kwa ajili ya kulumbana na serikali wala BOT ila wanaomba kupewa nafasi na viongozi hao ili waeleze namna gani wanaendesha kampuni yao.
“Tunaomba tualikwe tujieleze kwa rais, waziri mkuu na BOT kwa nini sisi sio upatu, DECI tuna mfumo unaoeleweka tofauti na taasisi nyingine ambazo hazijasajiliwa…tunahukumiwa sisi hivi hivi tu wakati lengo letu ni kukwamua wananchi wa chini kutoka katika umasikini,” alisema.
Kipili alisema wanaishukuru serikali na BOT kwa kutoa tangazo lake maana inaoonyesha kuwa inawatazama na inania ya kuona chombo hicho kinakaa katika utaratibu unaotakiwa pamoja na mapungufu yaliyojitokeza.
Wakti huo huo....................
ASKOFU Mkuu wa FGBF, Zachary Kakobe amewataka viongozi wa dini kutotafsiri maandiko ya biblia kwa maana nyingine kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kuleta uvunjifu wa amani na zaidi kuwachukulia hatua wote wanaovunja sheria za nchi pasi kuwabembeleza.
Aidha amewakata waliokwenda kuweka fedha na kuvuna katika Kampuni ya Development Entrepreneurship For Community Initiative (DECI) kuchukua fedha zao mapema kabla fedha hizo havijaingia kwenye viroba vya mikono ya watu walioanzisha kwa maslahi yao.
1 comment:
Mkuu,
Mie nilishasema tangu awali kuwa utatuzi wa tatizo unaweza kuleta mtafaruku. Mark my words! Yangu macho.
Mdau
Faustine
Post a Comment