Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), umeipa rungu kampuni ya mnada ya Majembe Auction Mart kusimamia shughuli zote za usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam.
Kampuni hiyo imepewa jukumu la kuhakikisha kuwa inawashughulikia madereva wachafu, wanaokatisha ruti, wanaopandisha nauli wakati wa usiku pamoja na kupita kwenye hifadhi ya barabara.
Aidha, makosa mengine ambayo kampuni hiyo itayashughulikia ni pamoja kukamata magari yaliyotoboka chini, wanayotoa moshi na mambo mengine yote yanayovunja sheria za barabarani.
Uamuzi huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israeli Sekilasa, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Sekilasa alisema kampuni hiyo itafanya kazi sambamba na jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa usafiri katika jiji la Dar es Salaam unaboreka.
Alisema ubabaishaji katika shughuli za kuendesha biashara ya daladala umefikia mwisho na ............
SOURCE: NIPASHE
Tujadili..
Pamoja na nia nzuri ya SUMATRA lakini hii inaonesha au ina maanisha nini?
Kwa mtazamo wangu ni kuwa, kwanza ni kama vile SUMATRA na Jeshi la polisi wameshindwa kabisa kuwadhibiti Daladala na hii ni dalili ya kusarenda kwa Daladala, jambo ambalo nathani halina mustakbali mwema mbeleni, swali ni kwa vipi au ni kweli kuwa wameshindwa au kuna sababu zilizojificha nyuma ya kushindwa kwao?
Pili naamini Jeshi la polisi linawatendaji wengi na nguvu za kisheria ama mabavui kuliko Majembe lakini bado limeshindwa kuwadhibiti, Je Majembe wana watendaji wa kutosha? na je watakuja na mbinu gani mpya kuweza kuwadhibiti hao daladala? kwani vituo ni vingi na Daladala ni nyingi mno.
Tatu mkataba huu ukoje? ni nani analipa gharama za hawa Majembe na kwa kiasi gani kwa siku ama kwa mwezi na atimaye mwaka wa mkataba? pengine ni hao hao daladala, kwa maana faini yasemekana yaanzia laki 2 papo hapo, lakini je SUMATRA si walikuwa na faini zinaanzia laki mbili na nusu? mbona hazikusadia kuondoa matatizo haya?
Wasiwasi wangu ama uzoefu onaonesha kuwa kadri faini ama kodi inapokuwa kubwa ndipo mwanya wa rushwa nao unapokuwa mkubwa pia, ni mtumishi gani atakataa kupokea elfu kumi au hamsini ili mtuhumiwa asilipe laki mbili za halali? iwapo askari wa barabarani na sumatra walishindwa ama walilazimishwa kushindwa sembuse Majembe? sijui labda hawa Vijana wa Kazi ni kizazi kipya katika Bongo chaweza kufanya miujiza, Tusubiri tuone.
No comments:
Post a Comment