Leo ktk vinjali yangu huku na huko mtandao ni niemebahatika kukutana na Blog ya Mh Mo Dewji, huyu ni Mbunge wa Singida Mjini Mjumbe wa CCM NEC, Mfanyabiashara maarufu, Mwanamichezo na Mmiliki wa timu pia, pamoja na shughuri nyingi zote hizi bado kaona umuhimu wa kuwa na jukwa la kubadilishana mawazo yaani Blog, akiwa na lengo kubadilisha na mawazo na wabongo na wana blog woote duniani hakika ulimwengu wa blog si mdogo kama baadhi ya watu wanavyodhani, bali njia hii ya upashanaji habari, uelimishanaji na burudani ni mpana na wahusisha watu wengi sana na ni njia rahisi sana ya kufikisha ujumbe kwa jamii inayo kuzunguka.
Rais wa Marekanai Barack Obama juzi alichukua muda kumjibu mwanablog Yoani Sanchez wa Cuba (angalia post hapo juu), baada ya dada huyo kupost maswali kadhaa kwa Obama kwenye blog yake. (sina hakika kama hicho chawezekana kufanyika hapa Bongo pia)
Karibu sana Mo Dewji, lakini jambo mmoja (sijui ni tatizo au) la kublog ni kukubali kuwa mtumwa wa blog au wadau maana haka ni kama kaulevi fulani hivi kila siku wahisi wawiwa na kitu iwapo inapita bila kupost au kutyembelea bloguni kuona watu wame-coment nini au kuna kitu gani kipya.
No comments:
Post a Comment