May 1, 2009

Kidato cha sita matokeo "out"

BARAZA la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita (ACSEE) uliofanyika Februari mwaka huu ambapo kiwango cha ufaulu kimeongezeka, huku shule za serikali za vipaji maalumu ziking’ara katika 10 bora.
Katika matokeo hayo pia kiwango cha ufaulu kwa wasichana kimeongezeka ikilinganishwa na wavulana huku katika wanafunzi 10 bora kitaifa, akijitokeza msichana pekee, Sophia Nahoza kutoka Sekondari ya Wasichana ya Marian mkoani Pwani.
Ndalichako alizitaja shule 10 bora zenye watahiniwa zaidi ya 25 na mikoa zilizo katika mabano kuwa ni Kibosho wasichana (Kilimanjaro), Marian wasichana (Pwani), Kibaha vipaji maalumu (Pwani), Mbumbe vipaji maalumu (Morogoro), Ilboru vipaji maalumu (Arusha), Malangali (Iringa), Maua Seminari (Kilimanjaro), Uru Seminari (Kilimanjaro), St Mary Goreti (Kilimanjaro) na Boniconsili Mabamba wasichana (Kigoma).
‘Zilizoshika mkia’ katika kundi hilo kwa kuanzia na ya mwisho ni Ambassador (Dar es Salaam), Maswa wasichana (Shinyanga), Dodoma Central (Dodoma), Fidel Castro (Pemba), Muslim College (Zanzibar), Uweleni (Pemba), Tumekuja (Zanzibar), Popatlalis (Tanga), Dk. Olsen (Manyara) na Jaffery (Arusha).

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...