MTUHUMIWA wa 11 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa Mahenge mkoani Morogoro inayomkabili aliyekuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe.Rashid Lema,amefariki dunia leo Alfajiri.
Lema anayedaiwa kuchangia kukamatwa kwa Zombe kutokana na kutoa maelezo yanayomhusisha,amefariki katika Taasisi ya Saratani Ocean Road na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali hiyo.
Marehemu Lema na Watuhumiwa wenzake 12 wanadaiwa kuwaua Ephraim Sabinus Chighumbi, Sabinus Chighumbi, Alias Jongo, Mathias Lung’ombe na Juma Ndugu ambaye alikuwa dereva teksi na mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Januari 14, mwaka 2006 katika msitu wa Pande, Mbezi Lusi wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Je kifo hiki chamaanisha nini ktk kesi hii iliyovuta hisia kubwa kwa jamii?
Taarifa zasema ushaidi wake ulikuwa muhimu sana katika kesi hii, je kwa kufa kwake ina maana na ushaidi wake umekufa au vipi???
Wadau wataalamu wa sheria naomba michango yenu katika hili??
No comments:
Post a Comment